Wataka viwanda vya alizeti viwiane na kilimo

ONGEZEKO la viwanda vya kusindika mafuta ya alizeti limetakiwa kwenda sambamba na kasi ya ulimaji wa zao hilo ili kunusuru viwanda na ukosefu wa malighafi. Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Dk Vedastus Timoth, Wakala wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO), wakati wa ziara ya Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.

Add a comment