HabariLeo | Gwiji la Habari Tanzania http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa Thu, 30 Oct 2014 19:22:59 +0300 Joomla! - Open Source Content Management en-gb Ajali ya Hiece yaua 12 Arusha http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31451-ajali-ya-hiece-yaua-12-arusha http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31451-ajali-ya-hiece-yaua-12-arusha

WATU 12 wamekufa papo hapo katika ajali iliyotokea jana wilayani Arumeru, Arusha ikihusisha basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace na lori la mafuta, aina ya Scania. Ingawa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas hakupatikana kuzungumzia tukio hilo licha ya mara kadhaa kupigiwa simu yake ya kiganjani iliyoita bila ya kupokewa, mwandishi wa habari hizi alishuhudia miili ya watu hao ikipokewa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, majira ya saa 12 jioni.

]]>
bmsongo@hotmail.com ( John Mhala, Arusha ) Habari za Kitaifa Thu, 30 Oct 2014 06:43:47 +0300
SMS ya nabii yavunja ndoa ya muumini wake http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31437-sms-ya-nabii-yavunja-ndoa-ya-muumini-wake http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31437-sms-ya-nabii-yavunja-ndoa-ya-muumini-wake

UJUMBE mfupi wa simu ya mkononi (SMS) wa kimapenzi ambao ulitumwa kutoka simu inayomilikiwa na kiongozi wa kanisa la Ngurumo ya Upako, Nabii Geor David Kasambala kwenda kwa mke wa muumini wa kanisa hilo umesababisha ndoa kuvunjika. Mwanamke aliyetumiwa SMS na nabii huyo ni Pamela Godfrey, mke wa Wilson Lota, wote waumini wa kanisa linaloongozwa na Nabii Geor David.

]]>
bmsongo@hotmail.com (John Mhala, Arusha ) Habari za Kitaifa Thu, 30 Oct 2014 05:58:58 +0300
JK ashtushwa kifo cha Rais wa Zambia http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31435-jk-ashtushwa-kifo-cha-rais-wa-zambia http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31435-jk-ashtushwa-kifo-cha-rais-wa-zambia

RAIS Jakata Kikwete ameelezea kuguswa, kushtushwa na kusononeshwa na taarifa za kifo cha Rais wa Zambia, Michael Chilufya Sata kilichotokea juzi Jumanne katika Hospitali ya King Edward VII, London, Uingereza, ambako alikuwa anatibiwa akiwa na umri wa miaka 77. Katika salamu zake alizomtumia Makamu wa Rais wa Zambia, Dk Guy Scott kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Rais Kikwete amesema:

]]>
bmsongo@hotmail.com (LUSAKA, Zambia ) Habari za Kitaifa Thu, 30 Oct 2014 05:58:55 +0300
NSSF kuunganisha Dar – Zanzibar kwa daraja http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31436-nssf-kuunganisha-dar-zanzibar-kwa-daraja http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31436-nssf-kuunganisha-dar-zanzibar-kwa-daraja

BAADA ya ndoto ya kuziunganisha pande mbili za katikati ya Jiji la Dar es Salaam na Kigamboni kwa daraja lenye umbali wa meta 680, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linaangalia uwezekano wa kujenga daraja la kihistoria zaidi litakalounganisha Dar es Salaam na Zanzibar.

]]>
bmsongo@hotmail.com (Katuma Masamba ) Habari za Kitaifa Thu, 30 Oct 2014 05:51:57 +0300
Makazi ya watuhumiwa wizi wa mifugo yateketezwa http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31439-makazi-ya-watuhumiwa-wizi-wa-mifugo-yateketezwa http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31439-makazi-ya-watuhumiwa-wizi-wa-mifugo-yateketezwa

WATU wasiojulikana wamevamia na kuchoma zaidi ya nyumba 10 za watuhumiwa watano wa wizi wa mifugo na wengine wanaojihusisha na migogoro ya ardhi wilaya ya Rorya mkoani Mara.

]]>
bmsongo@hotmail.com (Samson Chacha, Rorya ) Habari za Kitaifa Thu, 30 Oct 2014 05:50:06 +0300
Umasikini nchini wapungua zaidi http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31438-umasikini-nchini-wapungua-zaidi http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31438-umasikini-nchini-wapungua-zaidi

HALI ya umasikini nchini imepungua kutoka asilimia 34 hadi kufikia asilimia 28.2 ya Watanzania, ambao sasa ndio ambao wanaelezwa kuwa ni masikini zaidi, kutokana na kuishi chini ya Sh 1,216 fedha ambazo ndio uwezo wao katika kukidhi mahitaji yao ya msingi ya kila siku.

]]>
bmsongo@hotmail.com (Shadrack Sagati ) Habari za Kitaifa Thu, 30 Oct 2014 05:48:45 +0300
Kamati ya Bunge yaibana Wizara ya Ardhi http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31452-kamati-ya-bunge-yaibana-wizara-ya-ardhi http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31452-kamati-ya-bunge-yaibana-wizara-ya-ardhi

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeitaka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kutengeneza mpango wa upimaji maeneo ya makazi yasiyopimwa nchini ili yatambuliwe rasmi, lengo ni kuhakikisha serikali inakusanya fedha za kodi ya ardhi inayopotea, kutokana na nyumba nyingi kukosa hati ya umiliki.

]]>
bmsongo@hotmail.com (Ikunda Erick ) Habari za Kitaifa Thu, 30 Oct 2014 05:38:55 +0300
Hukumu kesi ya kutishia kumuua Mbunge http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31420-hukumu-kesi-ya-kutishia-kumuua-mbunge http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31420-hukumu-kesi-ya-kutishia-kumuua-mbunge

HUKUMU ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, Anthony Mahwata ya kutishia kumuua kwa maneno Mbunge wa zamani wa Jimbo la Njombe Magharibi, Yono Kevela imepangwa kuwa Novemba 27, mwaka huu.

]]>
bmsongo@hotmail.com (Mwandishi Wetu, Njombe ) Habari za Kitaifa Thu, 30 Oct 2014 05:16:31 +0300
'Kidato cha nne msiibe mitihani' http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31414-kidato-cha-nne-msiibe-mitihani http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/31414-kidato-cha-nne-msiibe-mitihani

WANAFUNZI wa Kidato cha Nne wanaotarajiwa kufanya mtihani wa taifa wameonywa kujiepusha na vishawishi vya kushiriki kwenye wizi wa mitihani na udanganyifu mwingine utakaowaondolea sifa ya kuendelea kufanya mitihani yao.

]]>
bmsongo@hotmail.com (John Nditi, Morogoro) Habari za Kitaifa Thu, 30 Oct 2014 05:00:24 +0300