IPAD - KUKABIDHI.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akikabidhi Ipad tano kwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Jackson Msome kwa ajili ya matumizi ya maofisa habari wa mkoa wa Kagera. Msome alikuwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu, Salum Mustafa Kijuu. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment

Kengele

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya nishati ya teknolojia ya umeme ya ABB, Leon Viljoen (kushoto), akigonga kengele kuashiria uzinduzi wa karakana ya kisasa ya utengenezaji wa vifaa mbalimbali vya umeme jijini Dar es Salaam jana. Nyuma yake ni Mkuu wa Kitengo cha Ufundi wa ABB Tanzania, Leonard Marango na Mkurugenzi Mtendaji wa ABB Tanzania, Michael Otonya. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment

Abiria

Ofisa Mawasiliano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro (kulia) akimkabidhi zawadi na tiketi abiria wa millioni mbili wa Fastjet, Peace Mteketa alipowasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam akitokea Nairobi juzi. Shirika hilo lilifikisha abiria wa millioni mbili tokea lianze safari zake ndani na nje ya Tanzania. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment

Bunduki

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi, Damasi Nyanda akionesha bunduki aina ya SMG iliyokamatwa katika operesheni maalumu pamoja na magazini mbili na risasi 86. Katika operesheni hiyo watuhumiwa wanne wanaosadikiwa kuwa majangili sugu walikamatwa. (Picha na Peti Siyame).

Add a comment

Ofisi

Ofisa Ugavi Kampuni ya Simu ya Airtel, Teddy Mkizungo akishiriki ujenzi wa ofisi ya walimu inayojengwa kwa hisani ya wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika shule ya msingi Mbezi Juu iliyopo Goba, jijini Dar es Salaam juzi. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment