Yanga cheko la ubingwa

YANGA jana ilijisogeza jirani na ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga Tofo Africans mabao 2-1 Uwanja wa CCM, Kirumba Mwanza. Ushindi huo umeiwezesha timu hiyo kufikisha pointi 65 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kucheza mechi 26, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 58 na Simba yenye pointi 57.

Add a comment

Simba, Azam wabanana Dar

LEO ni Simba na Azam kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zote zikiwania ubingwa wa Ligi Kuu unaoshikiliwa na Yanga. Azam inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kufikisha pointi 58 pointi saba nyuma ya vinara wa ligi Yanga yenye pointi 65 na ikiiacha Simba inayocheza nayo leo kwa tofauti ya pointi moja.

Add a comment