19Aprili2014

 

Margareth Kenyatta: Mke wa Rais anayetumia riadha kuokoa wanawake, watoto

ASUBUHI ya Aprili nane mwaka huu wakati napitia mitandao mbalimbali ikiwemo ya Kenya, niliona tangazo kuhusu mahojiano kati ya watangazaji wa kituo cha televisheni cha Citizen na Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo ambayo yangerushwa usiku wa siku hiyo.

Soma zaidi...

  • Imeandikwa na Basil Msongo
  • Imesomwa mara: 0

Milionea aliyekutana na 'miiba’ katika maisha

AMA kweli mchumia juani hulia kivulini. Methali hii ina maana kubwa mno kwa Alex Mwita Msama, mmoja wa vijana wa mjini wenye umaarufu wa aina yake. Huyu ni mfanyabiashara na promota mahiri wa muziki wa injili ambaye kila zinapofika nyakati za sikukuu za kidini, hasa Pasaka, Krismasi na Mwaka mpya, hukutanisha umati mkubwa wa waumini wa dini hizo kupitia matamasha ya muziki aliyoyabatiza, ama Tamasha la Pasaka au Tamasha la Muziki wa Krismasi.

Soma zaidi...

  • Imeandikwa na Mwandishi Wetu
  • Imesomwa mara: 323

JUMA NKAMIA: Kutoka Mwalimu wa kujitolea hadi Naibu Waziri

BAADA ya kung’ara katika tasnia ya habari na utangazaji, hapa nchini na nje ya nchi, hivi sasa ni miongoni mwa watu waliojitengenezea historia ya maisha hapa nchini. Hii ni kutokana na yeye kujiunga katika shughuli za kisiasa.

Soma zaidi...

  • Imeandikwa na Nashon Kennedy
  • Imesomwa mara: 398

Msamaria anayetumia facebook kuokoa watu

PICHA ya mtoto Rukia Rajabu ilileta simanzi kubwa. Kila aliyeiona alisikitika na kuomba apone. Kazi ya Mungu haina makosa. Mtoto Rukia alifariki siku chache baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Nyangao, mkoani Lindi. Victor Richard, mwenye umri wa miaka 35, mume na baba wa watoto watatu, alipigania uhai wa mtoto huyo kupitia mtandao wa kijamii wa facebook mithili ya mwanawe.

Soma zaidi...

  • Imeandikwa na Stella Nyemenohi
  • Imesomwa mara: 354

Nyota wa Simba, Taifa Stars aliyegeuka `nabii’ Marekani

HAKUNA shaka kwamba, kwa yeyote anayesikia jina la Nteze John Lungu moja kwa moja akili yake ataihamishia katika soka. Hii inatokana na ukweli kwamba, enzi zake alikuwa na umahiri wa kipekee katika kusakata soka, akiimudu vyema nafasi ya ushambuliaji kiasi cha kuwa tegemeo katika kila timu aliyoichezea. Wengi wanayakumbuka makali yake kuanzia akiwa na klabu za Pamba ya Mwanza, Simba, Kajumulo na hata timu ya taifa ya Tanzania `Taifa Stars’.

Soma zaidi...

  • Imeandikwa na Eric Anthony
  • Imesomwa mara: 692