22December2014

 

Wakulima hawa wa Kishapu wachukuliwe hatua

ZAO la pamba hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Geita, Simiyu, Mara, Tabora na Singida.

Read more...

 • Written by Mhariri
 • Hits: 38

Tusiache eneo la Rufi ji kugeuka Kilosa nyingine

LEO hii katika gazeti letu tumeandika fukuto la mgogoro wilaya ya Rufiji mkoani Pwani, ambalo wakati wowote unaweza kuzua mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika eneo ambalo, simulizi la aina hiyo halijawahi kufikirika tangu kuanza kwa historia ya Tanzania.

Read more...

 • Written by Mhariri
 • Hits: 93
Tahariri

Yanga, Simba zijitafakari

KATIKA maoni yetu ya gazeti hili Jumamosi iliyopita, tulionya kuhusu pambano la Nani Mtani Jembe 2 kutumika kuwafukuza makocha wa timu zilizokuwa zikimenyana siku hiyo, Yanga na Simba.

Read more...

 • Written by Mhariri
 • Hits: 135

Adhabu hii ya wakurugenzi iwe fundisho

JUZI Serikali ilitoa taarifa juu hatua ilizochukua dhidi ya wakurugenzi 17 wa halmashauri mbalimbali nchini baada ya kushindwa kutimiza wajibu wao katika kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika Jumapili iliyopita.

Read more...

 • Written by Mhariri
 • Hits: 236

Trafiki ongezeni juhudi wakati huu

JUZI gazeti hili lilikuwa na habari kuhusu kampeni inayoendelea nchini, inayowataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Kampeni hiyo inaendeshwa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na kampuni ya Vodacom Tanzania na Baraza la Taifa la Usalama  Barabarani.

Kampeni hiyo ilizinduliwa wiki iliyopita na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe, jijini Dar es Salaam na sasa inaendeshwa huko mikoani.

Tunaunga mkono kampeni hiyo, kutokana na ukweli kuwa wakati huu wa mwishoni mwa mwaka, watu wengi wanasafiri kutoka mijini kwenda vijijini kwao kuungana na familia zao kusherehekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Katika kampeni hiyo, madereva wanaagizwa kuacha kutumia vinywaji vyenye kilevi na kuacha tabia ya kuzungumza na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno wa simu (SMS) wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.

Ni dhahiri kama madereva wengi, wakiacha kufanya mambo hayo matukio ya ajali yatapungua. Tunashauri madereva wazingatie maelekezo hayo kwa usalama wao na wa abiria wanaowabeba, hasa wakati huu ambao maelfu ya watu watasafiri kwenda kwao na muda mfupi ujao, watarejea tena mijini.

Uzoefu umeonesha kuwa madereva wakizingatia sheria za barabarani, kwa kiasi kikubwa ajali hupungua. Aidha, tunapongeza kampuni ya Vodacom kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na tatizo la ajali za barabarani, ambalo limekuwa sugu nchini.

Tunaomba makampuni mengine ya simu kuiga mfano wa Vodacom na kuisaidia serikali kupambana na ajali za barabarani, ambazo zinaua watu wengi na kuacha wengine vilema.

Kwa upande wao, wasafiri nao inabidi kuisaidia serikali kutoa taarifa ya matukio yote ya uzembe na ukiukaji wa sheria za barabarani, unaofanywa na madereva, kwa polisi wa usalama barabarani (trafiki) na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA).

Wasafirishaji na madereva wote ‘wanaochakachua’ safari ni lazima waripotiwe trafiki na polisi ili wakamatwe. Ni vyema polisi na trafiki wahakikishe kuwa abiria wanatozwa nauli halali na mabasi hayo yanakaguliwa kwa kina yanapoanza safari na katika vituo vya ukaguzi, vilivyopo njiani.

Idadi ya trafiki wanaokaa barabarani ni vema iongezwe maradufu na vifaa vyote vya kuwapima madereva, vipatikane kwa wingi na wadhibitiwe ipasavyo njiani hadi mwisho.

Pia, serikali iwafuatilie kwa karibu tatizo la upungufu wa mabasi kutoka Dar es Salaam kwenda katika mikoa ya Mwanza, Kigoma, Mbeya, Ruvuma, Shinyanga, Rukwa, Mara na Tabora, ulioanza kujitokeza hivi sasa.

Lazima uchunguzi ufanywe kwa wale wote waliopewa leseni ya mabasi ya kutoa huduma katika ruti hizo na watakaobainika kutaka kujinufaisha na kipindi cha sasa, wadhibitiwe kama wanaolangua tiketi.

Ni imani yetu kila mmoja atajitahidi kuwezesha Watanzania kusherehekea vizuri sikukuu hizi za mwisho wa mwaka.

 • Written by Mhariri
 • Hits: 156

Mkutano huu wa hifadhi ya jamii uwe na tija kwa taifa

SERIKALI kupitia Wizara ya Fedha imeitisha mkutano mkubwa wa kimataifa mjini Arusha, wenye lengo la kuchota maarifa kutoka nchi nyingine namna ya kuwezesha sera bora za hifadhi.

Read more...

 • Written by Mhariri
 • Hits: 175