Makonda tusaidie watembea kwa miguu

KWA muda sasa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Saalam kumekuwa na kero hasa kwenye njia za watembea kwa miguu kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga kupanga bidhaa zao katika maeneo ya barabara. Hali hii ipo katika maeneo mengi ya jiji hili na kero zaidi huwa katika maeneo yenye vituo vikuu vya daladala au maeneo ambayo ni ya kibiashara.

Add a comment