EWURA Banner
HabariLeo Logo
 
Tafuta:
 
 
 
Habari za Kitaifa

Balaa lingine kwa Chenge
Imeandikwa na Halima Mlacha; Tarehe: 27th March 2009 @ 20:30 Imesomwa na watu: 21793; Jumla ya maoni: 14


Habari Zaidi:
  • Mgombea ajitangaza kuwakilisha vyama viwili
  • CCM wahimizana kuvunja kambi
  • Chadema Moro waanza nyumba kwa nyumba
  • Kingunge: Watanzania kuchagua wagombea waaminifu
  • Ofisa Ugavi mbaroni kwa tuhuma za kughushi
  • Askari waadhimisha miaka 46 JWTZ kwa kujitolea damu
  • Bakwata yataka ufafanuzi wa ‘hukumu ya baraghashia’
  • Tigo yaja na Tigo Pesa
  • Ewura yapata mwarobaini wa uchakachuaji mafuta
  • Mfuko wa Pembejeo Wilaya wawa kikwazo kwa wakulima
  • Mbeya kutahini darasa la saba 77,142
  • Ndege yaanguka Rukwa
  • Kikwete azidi kumwaga ahadi
  • Slaa kupunguza posho za wabunge, VAT
  • Mkameruni akamatwa na dola bandia 74
  • Lori lamuua dereva wake
  • Mgombea CUF amuunga mkono Kikwete
  • CUF ikiingia madarakani kupandisha bei ya kahawa
  • Umoja wa Mataifa watoa mafunzo kwa wagombea
  • CUF walia hujuma katika kampeni

  • Habari zinazosomwa zaidi:
  • Balaa lingine kwa Chenge
  • Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
  • Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
  • ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
  • Vatican yamvua jimbo Askofu
  • Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
  • Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
  • Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
  • Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
  • JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
  • Aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge (61), amewekwa chini ya ulinzi katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar es Salaam, kwa zaidi ya saa saba baada ya kuhusishwa na ajali ya gari na bajaj ambayo imeua watu wawili. Waliokufa ni wanawake wawili ambao ndugu amejitokeza na kudai kuwa wote ni wageni, waliwasili juzi Dar es Salaam kutoka Mwanza na mmoja alikuwa njiani kwenda Zanzibar kuolewa. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, ajali hiyo ilitokea saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia jana wakati Chenge akiendesha gari namba T 512 ACE aina ya Toyota Hilux na kuigonga bajaj hiyo namba T 736 AXC iliyokuwa na abiria hao wawili wanawake.

    Chanzo hicho kilidai kuwa baada ya ajali hiyo, Chenge alikwenda kwanza nyumbani kwake na kuripoti kituoni hapo saa moja asubuhi jana na kuwekwa chini ya ulinzi na kuhojiwa hadi saa saba mchana, huku nje akisubiriwa na ndugu zake. Gazeti hili lilimshuhudia mbunge huyo wa Bariadi Magharibi akiingizwa kwenye gari la Polisi namba PT 0217 na kwenda eneo la tukio karibu na shule ya msingi ya Oysterbay katika makutano ya barabara za Karume na Haile Selassie, ambako alieleza namna ajali hiyo ilivyotokea.

    Wakati mbunge huyo akitolewa katika kituo cha Polisi, kulitokea vurugu baina ya ndugu zake na waandishi wa habari, ndugu hao wakitaka kuzuia Chenge kupigwa picha, hali iliyosababisha kusukumana na kurushiana maneno makali. “Ninyi mmezidi kumwonea huyu kwani ni lazima mumpige picha ndio muuze? Hebu tokeni hapa,“ alisikika mwanamke ambaye alikuwa mstari wa mbele kusukuma waandishi, huku akilia na almanusra wapigane na mmoja wa wapigapicha waliokuwa kazini.

    Hata hivyo, vurugu hizo zilimalizika baada ya waandishi kuwazidi nguvu ndugu hao na kung’ang’ania kumpiga picha mbunge huyo ambaye awali alikuwa akifunikwa magazeti na nduguze, lakini aliyatoa na kupisha waandishi wampige picha vizuri. Akiwa katika eneo la tukio, Chenge alimwelezea Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Peter Kivuyo, namna ajali hiyo ilivyotokea na alidai ilitokea baada ya bajaj hiyo kutaka kupita gari jingine kwa kasi.

    “Bajaj ile ilikuwa inataka kupita gari jingine lililokuwa likitoka Morogoro Stores, bahati mbaya kukawa na gari lingine linakuja, ile bajaj ikabana upande wangu na mimi nilikuwa katika mwendo wa kati ya kilometa 80 hadi 100 kwa saa,“ alidai Chenge. Alidai kuwa baada ya kuona bajaj ile inakwepa gari la mbele wasigongane uso kwa uso, alirudi upande wa kulia ndipo alipoigonga ubavuni kushoto. "Gari la nyuma lingesimama, dereva wake angeweza kueleza vizuri, ila baada ya ajali nikasikia watu wanaita 'Chenge! Chenge!’ nikajua niko salama, nikashuka,“ alidai.

    Aliendelea kudai kuwa aliposhuka, alikuta abiria wawili wanawake wakiwa bado wanapumua ingawa kwa shida, lakini walipofika trafiki hali zao zilizidi kuwa mbaya na katika kipindi hicho chote, dereva wa bajaj alikuwa haonekani. Naye askari wa usalama barabarani aliyefika katika ajali hiyo, Mustafa Salum, alimweleza Kivuyo juu ya tukio hilo, ambapo alisema alipata taarifa za ajali hiyo saa 10.30 alfajiri na alipofika eneo la tukio, alikuta tayari abiria hao wawili wameshafariki dunia. “Niliipeleka miili ya marehemu hospitali ya Mwananyamala, ila kwa mujibu wa watu waliokuwa eneo la tukio, waliowaona marehemu hao wawili katika ukumbi wa Maisha Club,“ alisema.

    Naye kaka wa mmoja wa marehemu hao, January Constantine, alisema alipata taarifa za kifo cha dada yake, Beatrice Constantine (34) asubuhi na alikwenda kutambua mwili wake hospitalini, lakini kutokana na alivyopondeka alimtambua kwa alama za mwili. Alisema dada yake ni mfanyabiashara na mkazi wa Mwanza na kwamba aliwasili Dar es Salaam, akiwa na rafiki yake huyo na ilikuwa aondoke jana alfajiri kwenda Zanzibar kwa ajili ya harusi ya rafiki yake huyo. Gazeti hili lilishuhudia gari la Chenge kwa mbele likiwa na damu, nywele na mabaki ya ubongo ambao unasadikiwa kuwa wa mmoja wa marehemu hao. Polisi pia iliokota kipande cha fuvu la mtu katika eneo la tukio.

    Gari hilo lilikuwa na stika ya Bima ambayo ilikatwa Juni 6, 2006 na kumaliza muda wake Juni 6, mwaka juzi. Naye Theopista Nsanzugwanko anaripoti kuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleiman Kova, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema mmiliki wa bajaj hiyo ni Zuwena Nassoro na anatakiwa kuripoti katika kituo chochote cha Polisi huku wakiwa wanamshikilia Chenge Oysterbay ili kuisaidia Polisi. Alisema uchunguzi wa tukio hilo unafanywa chini ya Kivuyo na wataalamu mbalimbali ili kuondoa dhana ya upendeleo kwa kuwa Chenge ni mtu maarufu.

    Chenge (62) alijiuzulu uwaziri wa miundombinu Aprili 20 mwaka jana, kutokana na kashfa ya rushwa ya dola milioni moja kutoka kampuni kubwa ya uuzaji vifaa vya kijeshi duniani ya BAE Systems. Alijiuzulu baada ya kudaiwa kupokea rushwa ili kuwezesha ununuzi wa rada ya kijeshi ya pauni milioni 20 za Uingereza na kwamba fedha hizo ziliwekwa katika akaunti yake ya kisiwa cha Jersey.

    Baada ya kujiuzulu, alikaririwa akisema pamoja na tuhuma hizo, mapenzi kwa nchi yake na chama chake, ndivyo vilimlazimisha achukue uamuzi huo na kuongeza kuwa fedha zilizokutwa katika akaunti yake hiyo hazina uhusiano wowote na BAE Systems. Tuhuma hizo za rushwa zilichochea kelele pale alipohojiwa na waandishi wa habari na kujibu kuwa fedha anazotuhumiwa nazo ni 'vijisenti (fedha kidogo)'.

     
         
     
    Jumla Maoni (14)
         
    Maoni   mi nasema waangalie ukweli uko wapi ikiwa ana makosa achukuliwe sheria na ikiwa hana basi wasimtie baba wa watu kitahanani kwani watamuua kwa presha na hao waliokufa nawapa pole wazee wao na wapoe kwani kazi ya Mungu haina makosa.
         
    Maoni   Tanzania imejaa na viongozi wala rushwa na hii kesi haitaenda popote, sijui lini wananchi watajifunza kutowachagua wala rushwa kuwa viongozi yaani upuuzi mtupu
         
    Maoni   Tangu mh.raisi aingie madarakani ni hotuba ya jana tu ambayo mimi binafsi ilinifanya niione taswira yake ya pili tukiachilia mbali ile ya sakata la makabidhiano ya gari la wagonjwa pale ikulu,hivi mh. raisi hii taswira yake aliyoionyesha jana huuionyesha kwa watendaji wake na wasaidizi wake wakaribu pale ambapo wanapo mpotosha,kumdanganya n.k,maana nilifurahishwa sana na ule mfano wake wa mbayuwayu na kong'ota"akili za kupewa changanya na zako" Je ushauri,maoni anayopewa na wasaidizi wake yeye huchanganya na yake?
         
    Maoni   Lakini jamani saa 10 za alfajiri, waheshimiwa kama yeye ukiachia akina abdalla, kwa kazi ngumu na makaratasi wanayokesha nayo si huwa wamelala ?

    Hebu tuwapimeni wanamaadili kweli ya uongozi hawa. Saa hizo urudi nyumbani tukutegemee asubuhi uwe fresh na mawazo ya kututetea ?
         
    Maoni   kauwa watu wawili na yeye auliwe na mkewe ua mwanawe mkubwa
    wapakiwe na bajaj gari liwagonge hakuna bahati mbaya siku sote muna muweka mtu kula na kuishi kosa amefanya na ushahidi upo watu wote wameona hukumu ni hapo hapo
    hi ni makusudi hakuna bahati mbaya
         
    Maoni   Wakubwa wa nchi hii wamezoea kuwadhulumu wanyonge. Kaiba mamilioni kawadharau wananchi na anajidai kuipenda nchi yake kwa sababu baba na mama yake hawafukui majalala ( majaa) kupata riziki. Masikini wanyonge wa nchi hii wanakufa kuijenga nchi yao wakubwa wanatembeza magari ya fahari na kuwatukana. Aaah! Masikini Watanzania.
         
    Maoni   Wakati umefika kwa jeshi la polisi kuwa makini na ufuatiliaji wa ukiukwaji wa sheria za barabarani na hasa katika kuhakiki uwezo wa madereva kutumia vyombo vya usafiri binafsi na abiria. Hii inawezekana kabla dereva hajapewa leseni na kwa ukaguzi wa mara kwa mara na wenye ufanisi.

    Kama maelezo ya muheshimiwa ni ya kweli basi dereva wa bajaji alikuwa na makosa na hatuna uhakika alikuwa na uwezo gani (mbali na kuwa na leseni) kama dereva. Na kwa nini madereva wetu wengi wanatoweka baada ya ajali kutokea? na kama hofu yao ni kuadhibiwa na wananchi wenye hasira kali kwanini wawaadhibu?

    Kuwa na uwezo wa kutumia vyombo vya abiria ni pamoja na kuhakiki chombo kama kinastahiki kuwa barabarani kwa wakati huo au la. kwanini kutumia gari ambalo bima yake imekwisha kwa muda mrefu? je gari hili lilikuwa likitumiwa wapi? na je kumbukumbu zake hazipo? Dereva anapoendesha gari lisilostahili kuwa barabarani ni kuhatarisha maisha yake na ya watumiaji wengine wa babarabara maana yamkini mawazo yake yatakuwa katita kuwakwepa askari wa usalama barabarani na siyo kuendesha.
         
    Maoni   Kilichopo wataalamu wa barabara waangalie kosa liko wapi, na watende haki sawa wasijewakaogopa eti kama ni huyo mheshimiwa ana kosa wataogopa kumtia hatiani.

    Lakini baba usiku unakwenda wapi ni wakati wa kupumzika, pia kutuliza akili yako ili uweze kutetea haki za wananchi.
         
    Maoni   unajua sisi viongozi tulishazoea kuwaonea na kuwadharau watu wa tabaka la chini cha kufanya inabidi kwanza uchunguzi wa kiina kufanywa na takukuru wahusishwe kwani atajaribu kutoa rushwa ili kuficha ukweli baada ya hapo sheria ifuatwe kama inavyo jieleza katika kifungu ............
    Nawasihi ndugu zangu tuwe na ubinadamu kwani kupewa cheo sio mwisho wa dunia ukadhania aliye chini hatokufikia kila kitu chapangwa na mwenyezi mungu twapaswa kumshukuru na kutenda kazi tuliyo pewa kufanya

    ashante
         
    Maoni   Sheria ifuate mkondo wake,likiisha hilo,bado la kuendesha gali ambalo bima yake imekwisha. Nawapa pole ndugu wa wafiwa,na nawausia subra.
         
    Maoni   hongereni sana kwa habari nzuri mje huku kwetu kilombero kuna mambo mengi ya kuyaripoti kwenye gazeti lenu
         
    Maoni   Mimi binafsi siwezi kumlaumu Mh. Chenge wala dereva wa bajaj maana kufanya hivyo ni kumuhukumu mtu bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha, kitu abacho ni kosa kufanya hivyo. Ila kwa uzoefu wangu, mimi kama dereva wa muda mrefu ni ukweli kwamba madereva wa bajaj wanapenda sana kuchomekea wanapokuwa barabarani kitu ambacho ni hatari kwao na habiria wanaotumia usafiri huo.
         
    Maoni   Watanzania tuna tabia mbaya ya kuhukumu wakati kuna chombo cha kuhukumu. Kwani Chenge ndio wa kwanza kufanya ajali na kusababisha kifo? Na ana tofauti gani na madereva waliofanya ajali za namna hiyo? Au Chenge ajali yake haikufanyika katika barabara ya kawaida? Nadhani hizo ni chuki binafsi. Tuiachie mahakama ifanye kazi yake.
         
    Maoni   Wataalamu wa barabara wapo.Mahakama ipo.Tuviache vyombo hivyo vifanye kazi yake bila kuingiliwa ili mwisho ujulikane. Kama Chenge atapatikana na makosa au mwenye bajaji basi sheria ichukue mkondo wake.
         
     
     
      Tuma Maoni yako
       

    Jina la Kwanza:

    Jina la mwisho:
    Baruapepe: Barua Pepe imekosewa.
    Maoni yako:   Andika Maoni yako tafadhali.Tafadhali andika Maoni yako.
     
     
     
    WAZO LANGU
    Image

    Magereza fanyieni kazi malalamiko ya wafungwa

    SOMA | HIFADHI
    SAFU
    Image

    Tekuteku za Tefutefu!

    SOMA | HIFADHI
    NYOTA WA WIKI
    Image

    Mtangazaji kajikomboa kwa kuanzisha redio

    SOMA | HIFADHI
    JISAJILI NASI
    Jina la kwanza:
    Jina la Ukoo:
    Baruapepe: A value is required.
     
     
     
    Wasiliana nasi mhariri@habarileo.co.tz, advertising@dailynews.co.tz
    Simu:+255 22 2 127492 au 22 2 116074 au +255 22 2 110595 au 22 2 127493
    HabariLeo © 2009 Haki zote zimehifadhiwa.
    DailyNews Building, Plot 7, Samora Avenue, Box 9033, Dar es Salaam, Tanzania Copyright © 2009 DailyNews Media Group
    Advertisement
    TSN Adveritising