HabariLeo Logo
 
Tafuta:
 
 
 
Habari za Kitaifa

Polisi:Mwakyembe hakupewa sumu
Imeandikwa na Kaanaeli Kaale; Tarehe: 17th February 2012 @ 23:26 Imesomwa na watu: 995; Jumla ya maoni: 3

 
Habari Zaidi:
  • Sitta, Makinda wawafunda wabunge wapya
  • Wahubiri Wakongo wapewa siku 7 kuondoka nchini
  • Benki ya Azania yahamisha makao makuu
  • Skytel yakarabati taa za Arusha
  • Wavuvi waapa kukabili uvuvi haramu
  • Hausigeli anayedaiwa kuua mtoto anusurika kifo
  • Vijana Chadema kumjadili Shibuda leo
  • Waziri Wasira apanda kizimbani
  • 'CAG fuatilia michango ya Mbagala'
  • Wakili atoa DVD kusaidia wafanyakazi kudai haki
  • Chadema vilio au shangwe leo
  • Mfanyabiashara adaiwa kuiba ubalozini
  • Kijana kizimbani kwa kulawiti watoto
  • Maduka ya kuuza vipuri yateketea Temeke
  • Ma- RC, Ma-DC watakiwa kuongoza, si kutawala
  • Wananchi waua watuhumiwa 3 wa ujambazi
  • Heineken yapata tuzo ya heshima ya afya
  • Mwalimu auawa kwa kupigwa na ubao usoni
  • 'Acheni kuingiza siasa kwenye miradi ya maendeleo'
  • Wawili mbaroni kwa mauaji ugomvi wa shamba

  • Habari zinazosomwa zaidi:
  • Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
  • Balaa lingine kwa Chenge
  • ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
  • Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
  • Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
  • Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
  • Vatican yamvua jimbo Askofu
  • JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
  • Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
  • Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
  • MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Kamishna Robert Manumba amesema taarifa za uchunguzi zilizofanywa na Jeshi la Polisi zinaonesha kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe hakupewa sumu.

    Manumba alitoa taarifa hiyo wakati wa kujibu maswali ya waandishi wa habari alipokutana nao jana Makao Makuu ya Polisi kutoa taarifa kuhusu mwenendo wa uhalifu nchini.

    Pamoja na mambo mengine, waandishi hao walitaka kujua hatua iliyochukuliwa na Jeshi la Polisi kuhusu madai yaliyotolewa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta kwamba Mwakyembe alipewa sumu.

    Kanumba alisema hata kabla ya madai ya Sitta, Jeshi la Polisi lilikuwa linafanya uchunguzi kuhusu madai ya Dk. Mwakyembe ya kupokea ujumbe wa kutishiwa maisha.

    "Kabla Mwakyembe hajaugua na kupelekwa India tulimhoji kuhusu malalamiko aliyowasilisha kwa maandishi kwamba alipokea ujumbe wa kumtishia maisha yake…pia tumeendelea kufanyia kazi tuhuma zinazotolewa na Sitta maana kuna jinai ndani yake,” alisema Manumba.

    Alisema katika uchunguzi huo, ofisi yake iliwasiliana na Wizara ya Afya kuomba taarifa za uchunguzi wa kisayansi kama ugonjwa wa Mwakyembe unatokana na kulishwa sumu.

    “Hata hivyo taarifa tuliyoipata kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaonesha kuwa ugonjwa uliokuwa unamsumbua Mwakwembe hautokani na kula chakula chenye sumu,” Manumba alisema.

    Alisema ofisi yake ikishakamilisha kuandika ripoti ya uchunguzi itaiwasilisha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini.

    Waandishi wa habari walipotaka kufahamu kama Waziri Sitta atashtakiwa kwa kutoa habari zisizokuwa na ukweli, Manumba alisema Sheria ndio itaamua ashitakiwe au asishitakiwe. Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM) alikuwa mtu wa kwanza kuibua rasmi shutuma kuwa Dk. Mwakyembe, alikula chakula chenye sumu.

    Sitta ambaye ni rafiki na mshirika wa karibu wa Dk. Mwakyembe katika mapambano dhidi ya ufisadi nchini alitoa kauli hiyo katika mahojiano ya Kituo cha Televisheni cha ITV katika kipindi chake cha dakika 45.

     
         
     
    Jumla Maoni (3)
         
    Maoni   Inashangaza kuckia jeshi la polisi kutoa majib mepesi kiasi hicho wakati malalamiko ya awali ya Dr. Mwakyembe kuhusu njama za kuuwawa na kutaja majina ya watu mpaka gari la polisi na mganga wao wa kienyeji hayajashughulikiwa na hakuna dalili yoyote ya kushughulikiwa na tumeona baadhi ya wanaolalamikiwa wamehamishiwa mikoani ili kuziba ukweli wa kile kinacholalamikiwa. Hatuna jeshi bali tuna kampuni ya mafisadi.
         
    Maoni   UZUSHI NI HATARI KWANI KAMA DR.MWAKYEMBE ANGEZINGATIA USHAURI WA SITTA AKANYWA MADAWA YA KUFLASH SUMU AMBAYO HAIPO MWILINI HII INGEMPA MTIHANI WA KUFLASH MADAWA AMBAYO NAYO NI SUMU SASA SAMWELI SITTA ATAKUWA AMEFILISIKA KISIASA HUYU NI MCHOCHEZI SHERIA ICHUKUWE MKONDO WAKE ILA HANA SIFA YA KUWA WAZIRI
         
    Maoni   LINALO NISHANGAZA NI NANI MTAALAMU KUHUSU AFYA YA MGONJWA?JIBU RAHISI NI DAKTARI SASA HUYO MHESHIMIWA SITA HABARI YA SUMU YA MH MWAKYEMBE ALIZIPATA WAPI?HIYO INAONYESHA JINSI GANI TIBA MBADALA INVYO ENDEKEZWA.
         
     
     
      Tuma Maoni yako
       

    Jina la Kwanza:

    Jina la mwisho:
    Baruapepe: Barua Pepe imekosewa.
    Maoni yako:   Andika Maoni yako tafadhali.Tafadhali andika Maoni yako.
     
     
     
    WAZO LANGU
    Image

    Polisi ifanyieni kazi kauli ya Nchimbi

    SOMA | HIFADHI
    SAFU
    Image

    Unaifahamu mipaka yako katika uhusiano?

    SOMA | HIFADHI
    NYOTA WA WIKI
    Image

    FARID ABDALLAH: Mwanafunzi asiyeona kinara Kidato cha Sita 2012

    SOMA | HIFADHI
    JISAJILI NASI
    Jina la kwanza:
    Jina la Ukoo:
    Baruapepe: A value is required.
     
     
     
    Wasiliana nasi mhariri@habarileo.co.tz, advertising@dailynews.co.tz
    Simu:+255 22 2 127492 au 22 2 116074 au +255 22 2 110595 au 22 2 127493
    HabariLeo © 2009 Haki zote zimehifadhiwa.
    DailyNews Building, Plot 7, Samora Avenue, Box 9033, Dar es Salaam, Tanzania Copyright © 2009 DailyNews Media Group
    Advertisement
    TSN Adveritising