EWURA Banner
HabariLeo Logo
 
Tafuta:
 
 
 
Habari za Kitaifa

Ndoa zawagawa wabunge
Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 4th November 2009 @ 09:14 Imesomwa na watu: 1009; Jumla ya maoni: 8


Habari Zaidi:
  • Rushwa yawaponza polisi
  • Wasiofunga vidhibiti mwendo kukiona
  • Kapuya aagiza NSSF iiokoe CCM Kigamboni
  • Mshitakiwa 'kesi ya Magufuli' aaga dunia
  • Muswada wa Uchaguzi warudi kwenye Kamati
  • Mgombea binafsi bado kitendawili
  • Vyama ‘vidogo’ Z’bar vyachachamaa
  • Dereva Chatco kizimbani, akabiliwa na mashitaka 82
  • 'Utamaduni wasababisha kaya kuishi bila vyoo Pangani'
  • Kigoma waililia mitihani ya kata
  • Madereva sasa kupata leseni mpya Juni
  • Kinara 'form 4' afichua siri
  • Muswada wa uchaguzi moto
  • JK aagiza ujenzi Reli ya Kati uharakishwe
  • Anusurika kupigwa kanisani kwa wizi
  • Madereva 17 wa mabasi wafungiwa leseni
  • ‘Mradi wa vitambulisho vya Taifa sio wa kifisadi’
  • Wakataeni wanaotumia fedha kupata uongozi CCM - Pinda
  • Tendwa awaruka CCJ
  • Vitambulisho vya Taifa kutolewa mwaka huu

  • Habari zinazosomwa zaidi:
  • Balaa lingine kwa Chenge
  • Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
  • Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
  • Vatican yamvua jimbo Askofu
  • ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
  • Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
  • Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
  • Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
  • Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
  • JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
  • MBUNGE wa Kibakwe, George Simbachawene, amesema, kumzuia mtoto mwenye umri wa miaka 14 au 15 kuolewa kama yupo tayari kuhimili mikiki mikiki ya ndoa ni kumnyima haki yake ya msingi.

    Simbachawene amesema, si busara kumzuia mtoto kuolewa baada ya kuhitimu elimu ya msingi kwa kuwa si wote wenye malengo ya kuendelea na elimu.

    Mbunge huyo amesema, wapo watoto wenye umri wa miaka 16, ni mabinti wazuri wenye sifa za kuolewa. Kwa mujibu wa Mbunge huyo, jambo la msingi si kumzuia mtoto asiolewe, bali uthibitisho wa daktari kuwa anaweza kuingia kwenye taasisi hiyo.

    Simbachawene amesema, watoto wa kike wanakua haraka, hivyo wakiwa tayari kuolewa, wazazi washirikishwe ili wapate haki ya ndoa.

    Ameyasema hayo bungeni wakati anachangia muswada wa Sheria ya Mtoto wa mwaka 2009 unaohitimishwa leo.

    Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Lyimo, amesema, suala la umri wa kuolewa si la msingi kwa kuwa kuingia katika taasisi hiyo au kutoingia ni uamuzi wa mtu kwa kuzingatia mazingira husika.

    Mbunge wa Viti Maalum, Martha Mlata, amehoji, mtoto anayeolewa akiwa na umri wa miaka 14 au 15 anafuata nini huko?

    Kwa mujibu wa Mbunge huyo, kumruhusu mtoto mwenye umri huo aolewe ni sawa na kuruhusu watoto waoane.

    “Hivi unategemea nini akiwa leba… Ni ugonjwa huo kwamba anaenda kutibiwa?” amehoji Mbunge huyo wakati anachangia Muswada wa Sheria ya Mtoto wa mwaka 2009.

    “Mimi nakataa kabisa, na napinga sana” amesema Mbunge huyo na kupendekeza kuwa mtoto aolewe akifikisha umri wa miaka 18.

    Mbunge wa Viti Maalum, Diana Chilolo, amepinga kuruhusu watoto kuolewa na hasa wanapoolewa na wazee.

     
         
     
    Jumla Maoni (8)
         
    Maoni   Mimi kama mzazi nakubaliana kabisa na Mheshimiwa mbunge aliyekataa mtoto chini ya miaka 18 kuolewa. kwanza hata huyo wa hiyo miaka ni matatizo tu, kwani maisha ya ndoa yanahitaji kukomaa kiakili na uvumilivu. Mtoto chini ya huo umri hat viungo vyake havijakomaa kabisa kuhimili mikikimiki ya maisha.
    Asante
         
    Maoni   Kwa kweli ni muhimu kuwalazimisha watoto kufanya kile ambacho hawataki, mtoto wa miaka 14,15 kuolewa na kwenda kuendesha familia haifai kabisa, na isiruhusiwe kabisa, vingnevyo tutaruhusu utumbo, nakubali na iwe sheria, kuanzia miaka 18 ndo umri stahili kwa mtoto wa kike kuolewa.

    Na hata hao waoaji, kuoa mtoto kama huyo kisa ni nini?lazima pia waoaji wajiulize vyema katika hayo wanayoyafanya.

    Ahsanteni kwa kunisoma
         
    Maoni   UFANYIKE UTAFITI WA KUTOSHA KUONA KAMA TATIZO LIPO,NA LIPO KWA KIWANGO GANI ,SEHEMU TATIZO LILIPO KWA WINGI NA SABABU ZINAZOPELEKEA KUWEPO KWA TATIZO,Vinginevyo, haitasaidia kusema NDIYO au HAPANA,kwa sababu waoaji na waolewaji wanafanya hivyo kwa makubaliano yao na wakati mwingine kunakuwepo na baraka au msukumo wa wazazi. Kwa maoni yangu ni kwamba hata kama SHERIA itapitishwa kwa lengo zuri tu la kuwataka wanaoolewa watimize miaka 18 au zaidi,itafutwe na SHERIAmbadala itakayoweka umri wa mwanamke / mwanaume awe ameolewa/kuoa,Ugumu unaopatikana katika utekelezaji wa sheria mbadala itakayolazimisha kuolewa /kuoa ,ndio UGUMU wa aina hiyo unolazimisha watu watoe maoni ya NDIYO/HAPANA kwa umri wa miaka 14,15,au 18.
    Nashauri ELIMU ya kutosha itolewa kwa watu wote na hasa vijijini,iwe katika mfumo wa MFANO wa kisomo cha watu wazima iliyotolewa miaka ya sabini,kuwepo na TIME FRAME na jamii ipime matokeo ya elimu itakayotolewa kama itapunguza tatizo au kulimaliza tatizo.Kwa hiyo serikali itenge FUNGU kwa ajili ya shughuli hiyo.Vinginevyo maneno mazuri ya wanasiasa na hasa wabunge hayatasaidia kitu. mfano ni huu, NI MZAZI gani wa kijijini mwenye binti mzuri wa miaka 14 au 15 ambaye ATAMKATAA mfanyabiashara mwenye fedha au hata mbunge mwenye miaka 50 kumuoa binti yake, wakati mzazi huyo hana uhakika wa kupata hata mlo mmoja kwa siku ,HAYUPO MZAZI WA AINA HIYO, na mifano iko mingi katika NCHI YETU. We must find out THE CAUSE ROOT,AND NOT WHY THE CAUSE,and FIND a way on how to solve the PROBLEMS Scientifically through Research.
         
    Maoni   Jamani mmeshasema mtoto wa miaka 16 mnategemea nini katika hiyo ndoa atakayoenda? Je huyo mbunge anaetetea kuolewa mapema ana mtoto wa kike? ina maana mwanae akija kumwambia nataka kuolewa ( akiwa na miaka 16 atamkubalia?) SIDHANI
    Sheria hii mie naona iwe ni hapo atakapotimiza miaka 18 awe angalau akili imeanza kukomaa...

    Nimesikitika kusikia mbunge anatetea watoto kuolewa. Au akiambiwa mumewe anataka kuoa mtoto wa miaka 16 atakubali???

    SIO HAKI kwa watoto. Waacheni wawe watoto.

    Asante
         
    Maoni   suala la kuolewa wasichana wakiwa bado na umri mdogo nikuwatafutia wasichana matatizo wakati wa kujifungua kwani miili yao bado inakuwa haiwezi kuhumili mikiki na misukosuko ya uchungu. kwasababu hiyo wapo ambao tayari wamepoza maisha , wapo waliopata fistula na hata kuambukizwa magonjwa ya ukimwi na zinaa katika umri huo. Nakuomba mheshimiwa hoja hiyo isipewe nafasi kwa kigezo cha umaskini bali tunusuru maisha ya wasichana hao. suala la ndoa watalikuta tu muda wao ukifika. Nihayo sina mengi ya kuchangia.
         
    Maoni   Kuolewa ni uamuzi wa mtu.Kwa kawaida mtoto akishafika balehe tu anahisabika kakua.Akili za mtu haziwi nzuri kulingana na umri.Kuna watu wana umri zaidi ya miaka 30 lakini akili zao ni mbovu kabisaa na hawaisaidii jamii ya Tanzania kukua wanachofanya ni kuididimiza nchi.Kwa hiyo swala la kuolewa ni la mtu mwenyewe na si kumpangia sheria.Kuna mambo mengine yanayohusu nchi hii ambayo ni muhimu sana kuliko hili na yanahitaji kupewa ufumbuzi wa kina.Mfano swala la afya,utengenezaji hela sisi wenyewe,kukuza teknolojia kwa kutumia nguvu zetu wenyewe n.k. Huko nchi zilizoendelea wanasema mtu aolewe akiwa na zaidi ya miaka 18,lakini wengi wa watoto wanabeba mimba chini ya umri huo,fuatilia suala hili kwa nchi ya Marekani na Uingereza.Sasa lipi jema kubeba mimba ndani ya ndoa ambayo mtoto mwenyewe katoa maamuzi bila ya kulazimishwa au kubeba mimba kwa kufanya ngono nje ya ndoa ambapo ni chanzo cha ukimwi na umomonyoko wa maadili katika jamii?Tusiwe tunaiga kila sheria za nje, yabidi tuige lile tu lililo la kheri.Nafikiri tuwe na "free thinking mind, self determination".Cha msingi tu wazazi wawalee watoto vizuri na kuwaongoza.Lakini tukumbuke mtoto akibalehe tu si mtoto tena, yabidi kujali mawazo yake ili nchi iendelee.
         
    Maoni   Mtoto akifika kuhimili kuolewa na aolewe je na hao WANAOZINI na kupata mimba wakiwa chini ya umri wa miaka 18 mnasemaje hapo???? Ni bora kuzini au bora kuolewa???? aulizwe mtoto kama anapenda kuendela na masomo apewe haki ya kusoma na kama yupo tayari kuolewa basi na aolewe kuliko kufanya zinaa ambayo ni mbaya zaidi....
         
    Maoni   Hali ya maisha ya watanzania inatofautiana sana baina ya sehemu moja na nyingine, kuna watoto walioenda leba na miaka 13 wakazaa na kutoka salama na wapo walioenda na miaka 25 wakazaa kwa kisu. cha muhimu hapa mtoto kama ana miaka 14 na hasomi na yuko tayari kuolewea apewe haki hiyo, asikatishwe masomo wala asilazimishwe.

    Kama ukimkatalia kuolewa akapewa mimba itakuwa hasara ya nani? cha muhimu hapa ni elimu kwa wanandoa hao ili wajue kilichopo mbele yao.

    Mbona haitungwi sheria ya kuzuia wazee wasiowe mabinti wadogo ambao wengi wao hufa na kuwaacha watoto kwa mama zao maana umri wa kuishi wa kawaida kwao unakuwa umeshapita.

    Ahsante!
         
     
     
      Tuma Maoni yako
       

    Jina la Kwanza:

    Jina la mwisho:
    Baruapepe: Barua Pepe imekosewa.
    Maoni yako:   Andika Maoni yako tafadhali.Tafadhali andika Maoni yako.
     
     
     
    WAZO LANGU
    Image

    Kwa hili wabunge mnakumbatia rushwa

    SOMA | HIFADHI
    SAFU
    Image

    Bila nyumba huongozi!

    SOMA | HIFADHI
    NYOTA WA WIKI
    Image

    Mtangazaji, MC, mkufunzi wa ‘Kitchen Party’

    SOMA | HIFADHI
    JISAJILI NASI
    Jina la kwanza:
    Jina la Ukoo:
    Baruapepe: A value is required.
     
     
     
    Wasiliana nasi mhariri@habarileo.co.tz, advertising@dailynews.co.tz
    Simu:+255 22 2 127492 au 22 2 116074 au +255 22 2 110595 au 22 2 127493
    HabariLeo © 2009 Haki zote zimehifadhiwa.
    DailyNews Building, Plot 7, Samora Avenue, Box 9033, Dar es Salaam, Tanzania Copyright © 2009 DailyNews Media Group
    Advertisement
    TSN Adveritising