EWURA Banner
HabariLeo Logo
 
Tafuta:
 
 
 
Habari za Kitaifa

Sita wa familia moja wafa ajalini wakienda harusini
Imeandikwa na Na Hellen Mlacky, Same; Tarehe: 19th December 2009 @ 06:51 Imesomwa na watu: 1112; Jumla ya maoni: 5


Habari Zaidi:
  • Mgombea ajitangaza kuwakilisha vyama viwili
  • CCM wahimizana kuvunja kambi
  • Chadema Moro waanza nyumba kwa nyumba
  • Kingunge: Watanzania kuchagua wagombea waaminifu
  • Ofisa Ugavi mbaroni kwa tuhuma za kughushi
  • Askari waadhimisha miaka 46 JWTZ kwa kujitolea damu
  • Bakwata yataka ufafanuzi wa ‘hukumu ya baraghashia’
  • Tigo yaja na Tigo Pesa
  • Ewura yapata mwarobaini wa uchakachuaji mafuta
  • Mfuko wa Pembejeo Wilaya wawa kikwazo kwa wakulima
  • Mbeya kutahini darasa la saba 77,142
  • Ndege yaanguka Rukwa
  • Kikwete azidi kumwaga ahadi
  • Slaa kupunguza posho za wabunge, VAT
  • Mkameruni akamatwa na dola bandia 74
  • Lori lamuua dereva wake
  • Mgombea CUF amuunga mkono Kikwete
  • CUF ikiingia madarakani kupandisha bei ya kahawa
  • Umoja wa Mataifa watoa mafunzo kwa wagombea
  • CUF walia hujuma katika kampeni

  • Habari zinazosomwa zaidi:
  • Balaa lingine kwa Chenge
  • Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
  • Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
  • ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
  • Vatican yamvua jimbo Askofu
  • Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
  • Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
  • Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
  • Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
  • JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
  • WATU sita wa familia moja ni miongoni mwa watu 19 waliokufa katika ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Mohamed Trans lililogongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Asia Combi katika Kijiji cha Kandoto, nje kidogo ya mji wa Same mkoani Kilimanjaro juzi.

    Ndugu hao ambao wanatarajiwa kuzikwa leo katika Kijiji cha Mamba Kotela, Moshi Vijijini, walikuwa wakienda katika harusi ya Egbert Maleko iliyotarajiwa kufanyika leo kijijini humo.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko, ndugu hao ni pamoja na baba mdogo wa bwana harusi, Geoffrey Maleko (70), ) mkazi wa Mbezi na James Maleko (32) na mtoto wake, Mary James (6), wote wakazi wa Tabata Kisukulu, Dar es Salaam.

    Wengine ni Douglas Maleko na mkewe Grace Maleko (47) pia mkazi wa Kisukulu pamoja na baba mdogo wa bwana harusi, Mark Maleko (68) mkazi wa Tabata. Wote wanatarajiwa kuzikwa leo,harusi imeahirishwa.

    Aidha, maiti nyingine zilizotambuliwa katika ajali hiyo ni Hevenlight Minja, Neema Minja (13), Witness Minja (10) ambao nao ni ndugu wa familia moja; Glory Makundi mtoto mdogo wa miaka miwili na Johnson Moshi (15) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mabibo.

    Wengine waliotambuliwa ni utingo wa basi hilo aliyetambulika kwa jina moja la Simba na mtoto wa Parmina Mandame anayekadiriwa kuwa na miaka 20 hadi 26.

    Kamanda huyo wa Polisi alisema hali ya majeruhi watano waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Same inaendelea vizuri huku wengine waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC akiwemo fundi wa basi hilo, Hiza Mzungu na Greyson Maleko hali zao bado ni mbaya na wako katika wadi ya uangalizi maalumu (ICU).

    Majeruhi wengine ni Sia Maleko (31), Emmanuel Maleko (12), Hawa Dinny (39) mkazi wa Uingereza, Meela Moshi (30), mtawa Valentino Yonas (50), mkazi wa Tanga na Doreen Urio (46) mkazi wa Ilala; ambao wote wamelazwa katika Hospitali ya KCMC.

    “Mpaka sasa ni maiti 13 pekee ndio wametambuliwa na ndugu zao na maiti nyingine sita hawajatambuliwa hivyo tunatoa wito kwa wakazi wa Kiimanjaro kujitokeza zaidi ili kuweza kuitabua miili ya ndugu zao,” alisema.

    Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Same, Charles Kifunde, alisema kati ya majeruhi wote waliopokelewa 35 ambao walikuwa ni abiria wa basi la Mohamed Trans, walipatiwa matibabu na kuruhusiwa juzi kuendelea na safari baada ya kampuni hiyo kuwapa usafiri mwingine.

    Aidha, Rais Jakaya Kikwete jana aliwatembelea baadhi ya majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Same wakiwemo Joseph Akaro, Juta Molel, Waden Abdallah, Julieth Julius na Dorcas Moshi ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Vikindu, Mkuranga na kuwajulia hali.

    Ajali hiyo ilitokea juzi Kandoto nje kidogo ya mji wa Same na kuhusisha basi hilo lenye namba T810 AQM na gari dogo lenye namba T845 BCB lenye kufanya safari zake Sinza na Tandika, Dar es Salaam.

    Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi nchini limeunda kamati ya watu wanane kwa ajili ya kuchunguza mwenendo mzima wa jinsi mabasi ya Mohamed Trans yanavvyotoa huduma katika mikoa mbalimbali nchini.

    Msaidizi wa Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mtinga alisema hayo jana wakati akizungumza na gazeti hili, alipotakiwa kutoa tamko la jeshi hilo dhidi ya mabasi hayo.

    Alisema kamati iliyoundwa inahusisha Jeshi la Polisi pamoja na wadau wengine kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Majini na Nchi Kavu (Sumatra) ambapo itaongozwa na Kamishna wa Polisi Makao Makuu anayehusika na operesheni, Paul Chagonja na kwamba baadaye watatoa tamko rasmi.

    Mabasi ya Mohamed Trans yamekuwa yakipata ajali kubwa na mwaka huu, basi jingine linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Nairobi Kenya, liliua abiria 26 katika Kijiji cha Kwakombo, wilayani Korogwe, Mkoa wa Tanga, na mabasi hayo kuzuiwa kwa muda ili yakaguliwe, kabla ya kuruhusiwa kufanya tena safari.

     
         
     
    Jumla Maoni (5)
         
    Maoni   Nafikiri ni vizuri ukafanyika uutafiti wa kina kuhusu niaina gani ya matairi yanayotumika na Kampuni ya Mohamed Trans, pili madriva wake wachunguzwe kama wana liseni za uhakika au ni fake.
         
    Maoni   Tunawapa pole wote wafiwa, na marehemu mungu awalaze mahali pema peponi wako kutoka, LINDI JAMHULI
         
    Maoni   sasa manasema mtachukuza mabasi hayo .mimi nasema ni udereva tu maana hiyo picha inaonekana ni ajali ya mendo wa kasi si chini ya spidi ya 140 nadhani hayo mabasi ni mapya ndio maana madereva wanakwenda mbio fanyeni spidi limiti tu sio kuchuguza mabasi kama ni kuchuguza au ni mabovu sasa vipi yanaondoka kituoni angalieni umri wa madereva sio miaka 25 anapewa basi dereva wa basi awe na umri usio pungua 35 na usizidi miaka 60 na ulevi wa aina yoyote hata mirungi pia angalieni
         
    Maoni   Poleni sana.hayo mabasi mwisho wa kazi.hawawezi kuua ndugu hivyo!
         
    Maoni   Sina maoni ila majonzi kwa habari hii ya kusikitisha. Mwenyezi Mungu alaze Mahali Pema Peponi Roho za Marehemu hawa na pia awaponye majeruhi wote mapema. Amen.
         
     
     
      Tuma Maoni yako
       

    Jina la Kwanza:

    Jina la mwisho:
    Baruapepe: Barua Pepe imekosewa.
    Maoni yako:   Andika Maoni yako tafadhali.Tafadhali andika Maoni yako.
     
     
     
    WAZO LANGU
    Image

    Magereza fanyieni kazi malalamiko ya wafungwa

    SOMA | HIFADHI
    SAFU
    Image

    Tekuteku za Tefutefu!

    SOMA | HIFADHI
    NYOTA WA WIKI
    Image

    Mtangazaji kajikomboa kwa kuanzisha redio

    SOMA | HIFADHI
    JISAJILI NASI
    Jina la kwanza:
    Jina la Ukoo:
    Baruapepe: A value is required.
     
     
     
    Wasiliana nasi mhariri@habarileo.co.tz, advertising@dailynews.co.tz
    Simu:+255 22 2 127492 au 22 2 116074 au +255 22 2 110595 au 22 2 127493
    HabariLeo © 2009 Haki zote zimehifadhiwa.
    DailyNews Building, Plot 7, Samora Avenue, Box 9033, Dar es Salaam, Tanzania Copyright © 2009 DailyNews Media Group
    Advertisement
    TSN Adveritising