EWURA Banner
HabariLeo Logo
 
Tafuta:
 
 
 
Habari za Kitaifa

Shehe Yahya amtabiria JK ushindi 2010
Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 23rd December 2009 @ 23:59 Imesomwa na watu: 1548; Jumla ya maoni: 7


Habari Zaidi:
  • Mgombea ajitangaza kuwakilisha vyama viwili
  • CCM wahimizana kuvunja kambi
  • Chadema Moro waanza nyumba kwa nyumba
  • Kingunge: Watanzania kuchagua wagombea waaminifu
  • Ofisa Ugavi mbaroni kwa tuhuma za kughushi
  • Askari waadhimisha miaka 46 JWTZ kwa kujitolea damu
  • Bakwata yataka ufafanuzi wa ‘hukumu ya baraghashia’
  • Tigo yaja na Tigo Pesa
  • Ewura yapata mwarobaini wa uchakachuaji mafuta
  • Mfuko wa Pembejeo Wilaya wawa kikwazo kwa wakulima
  • Mbeya kutahini darasa la saba 77,142
  • Ndege yaanguka Rukwa
  • Kikwete azidi kumwaga ahadi
  • Slaa kupunguza posho za wabunge, VAT
  • Mkameruni akamatwa na dola bandia 74
  • Lori lamuua dereva wake
  • Mgombea CUF amuunga mkono Kikwete
  • CUF ikiingia madarakani kupandisha bei ya kahawa
  • Umoja wa Mataifa watoa mafunzo kwa wagombea
  • CUF walia hujuma katika kampeni

  • Habari zinazosomwa zaidi:
  • Balaa lingine kwa Chenge
  • Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
  • Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
  • ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
  • Vatican yamvua jimbo Askofu
  • Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
  • Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
  • Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
  • Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
  • JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
  • MTABIRI maarufu wa Afrika Mashariki, Shehe Yahya Hussein ametabiri kuwa Rais Jakaya Kikwete atashinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao na atakayempinga ndani ya chama chake atakufa ghafla.

    Sambamba na hilo, atakayeonekana kumshinda nje ya chama chake pia atapoteza maisha vivyo hivyo.

    Akitoa utabiri wake jana Dar es Salaam, juu ya uchaguzi mkuu mwakani, Shehe Yahya alisema ushindi wa Rais Kikwete unatokana kurithishwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1995 ilipodaiwa kuwa Rais Kikwete alishinda kwenye kura za maoni lakini akamsihi amwachie Benjamin Mkapa.

    Alisema ushindi wa Rais Kikwete unatokana na kutanguliwa kwa vifo vya watu waliotokea sehemu moja ambapo mwaka 2005 kabla ya uchaguzi, Mwenyekiti wa CCM Songea alifariki dunia na mwaka huu kabla ya uchaguzi tena kumetokea kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM , Lawrence Gama ambaye anatokea pia Songea.

    Alisema ushindi huo utaleta Serikali za mseto Tanzania Bara na Visiwani na kuongeza “kwa mara ya kwanza Waziri Mkuu ajaye atatokea Upinzani na kwa Zanzibar, CUF imeshaonekana kushinda”.

    Shehe Yahya alisema upinzani nje na ndani ya CCM utasambaratishwa na baadhi ya viongozi kujiunga na kambi ya Rais Kikwete wakiwamo wa Upinzani.

    Mtabiri huyo alisema kutokana na ushindi huo katika uchaguzi wa mwakani kwenda sambamba na vifo, kutatokea kifo cha kiongozi wa zamani wa kitaifa kati ya sasa na Aprili mwakani, kabla ya uchaguzi.

    “Kutatokea maandamano makubwa kupinga matokeo ya uchaguzi kuhusu wabunge wa pande zote wa CCM na Upinzani kuhusu wizi wa kura. Maandamano hayo yatasababisha kesi kubwa kupinga matokeo ya ubunge wa pande zote,” alitabiri.

    Katika utabiri wake huo wa mwisho wa mwaka huku akiahidi kutoa utabiri mwingine Januari 10 mwakani, Shehe Yahya alisema baadhi ya viongozi wa sasa wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere watajiuzulu kwa aibu itokayowafika kuihusisha taasisi hiyo na siasa ya kumpinga Rais Kikwete, ilhali taasisi hiyo ni ya watu wa pande zote na si ya siasa bali ya kusaidia kila mtu.

    Mtabiri huyo ambaye alijitapa kutabiri na matukio kuwa ya kweli ikiwemo ya kiongozi kupigwa kibao ambapo Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi alikumbwa na masahibu hayo, alisema mwakani pia kutatokea ajali nyingi kwa vyombo vya usafiri na pia hali ya uchumi kwa Watanzania itakua.

    Awali Msaidizi wa Shehe Yahya ambaye ni mtaalamu wa nyota, Abdulrahman Ally, akitoa utabiri wa nyota wa mwaka 2010 akisema utakuwa wa mabadiliko makubwa kwa watu watakaotawala nchi, huku mashindano makubwa kati ya mataifa yenye nguvu yakiongezeka.

    “Marekani itashuka katika wadhifa wake wa kidunia, huku mataifa madogo yanayokua yatakwaruzana na majirani zao, hii inaamanisha mwaka 2010 ni mwaka wa ugomvi kati ya nchi na nchi,” alisema.

    Ally alisema watu wa ibada, wanaozingatia uongofu kuliko uoga, wenye mapenzi dhidi ya chuki watakuwa na furaha kubwa mwakani.

     
         
     
    Jumla Maoni (7)
         
    Maoni   Naomba address ya sheikh Yahya Husain, I have met once in the flight from MUSCAT - DAR and unfortunatly I have lost his contact, could you please send me e-mail or telephone to get contact with him.

    your cooperation will be highly appreciated.
         
    Maoni   Mimi nawapongeza wote wanaotoa maoni,kwa vile wako makini kusoma habari hizi za kusisimua.Mimi Maoni yangu kama ifuatavyo;Huyu mzee nadhani anaoteshwa na ndoto za mchana.In short ni kujipendekeza tu kwa viongozi wa wakubwa ili aonekane yeye amechangia kiasi kikubwa ushindi huo wa mwaka 2010.Yote ni kutafuta pesa ya kujikimu,namaanisha hapa mjini bwana njia zingine za kutafutia pesa sio usimame Barabarani na kuomba.Hata njia hii unaweza kujipatia pesa 2.Mimi namshauri huyu mzee akae kimya tuangalie uchaguzi utakuaje.Sio kuropoka tu,yeye sasa ni mzee,kama yeye kidume,bora akaombe uwenyekiti wa ccm.
         
    Maoni   ahsante shehe yahya ! japokuwa mi ni miongoni mwa wasioamini mambo haya !
         
    Maoni   Muongo mkubwa huyo na mnafiki, kila siku anahubiri mambo ya ushetani na majini badala ya kuhubiri safari za mtume muhammad s.a.w na mawaidha yake. anataka kujipa ujiko tu. kwani nani asiyejua kuwa Kikwete ndio mwenye asilimia kubwa za ushindi, kuna haja ya kutabiri hilo?
         
    Maoni   nakupongeza sana sheh yahya kwa utabiri wako uliotukuka nadhani kwa wasioamini ni bora mkae kimya kulio kukosoa vitu ambavyo hamvijua lkn si neno binadamu kupinga kwani wamethubutu hata kumpinga tume na yesu kaza buti baba katika utbiri wako tunautegemea sana
    rabia
         
    Maoni   huyo mzee huwa anatabiri vya kweli hebu tusubiri huo uchaguzi wa mwaka 2010 jamani tuone!mimi sina tu adress yake wala namba yake ya simu naomba kupata namba yake ya simu jamani nataka nipo mbali na bongo ningeweza pata namba yake jamani?
         
    Maoni   kazi yake ni kuwatisha Binaadam huyu ni kiumbe mbaya sana kwani huwezi kumtabiria binaadam kufa wakati nawewe umeumbwa na huyohuyo aliyetuumba sasa wewe ni mungu wa Tz?Au yeye ndio huyo mwenye kuuwa albino?hata jina lake ni tafauti na yeye mwenyewe kama utamuona hakika unaweza kudhirai anatisha sio kiumbe wa kawaida,inawezekana yuko na viungo vya watu (ALBINO)Ni rafiki wa Rais wetu lakini inabidi tumtilie shaka kwa huwo urafiki wawo mpaka ikafika hadi kukutana na waandishi wa habari na kusema atii kama atatokea mtu ktk chama cha CCM na kutaka kugombea uraisi atakufa gafla.hayo hakika sio maneno ya kawaida.kazi kwako Padri anakusubiri kanisani ukatubu kwa hayo maovu yako kinyume chake mauti yatakukuta wewe kwanza!!.
         
     
     
      Tuma Maoni yako
       

    Jina la Kwanza:

    Jina la mwisho:
    Baruapepe: Barua Pepe imekosewa.
    Maoni yako:   Andika Maoni yako tafadhali.Tafadhali andika Maoni yako.
     
     
     
    WAZO LANGU
    Image

    Magereza fanyieni kazi malalamiko ya wafungwa

    SOMA | HIFADHI
    SAFU
    Image

    Tekuteku za Tefutefu!

    SOMA | HIFADHI
    NYOTA WA WIKI
    Image

    Mtangazaji kajikomboa kwa kuanzisha redio

    SOMA | HIFADHI
    JISAJILI NASI
    Jina la kwanza:
    Jina la Ukoo:
    Baruapepe: A value is required.
     
     
     
    Wasiliana nasi mhariri@habarileo.co.tz, advertising@dailynews.co.tz
    Simu:+255 22 2 127492 au 22 2 116074 au +255 22 2 110595 au 22 2 127493
    HabariLeo © 2009 Haki zote zimehifadhiwa.
    DailyNews Building, Plot 7, Samora Avenue, Box 9033, Dar es Salaam, Tanzania Copyright © 2009 DailyNews Media Group
    Advertisement
    TSN Adveritising