EWURA Banner
HabariLeo Logo
 
Tafuta:
 
 
 
Habari za Kitaifa

Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
Imeandikwa na Veronica Mheta; Tarehe: 25th April 2009 @ 00:01 Imesomwa na watu: 12820; Jumla ya maoni: 4


Habari Zaidi:
  • Mgombea ajitangaza kuwakilisha vyama viwili
  • CCM wahimizana kuvunja kambi
  • Chadema Moro waanza nyumba kwa nyumba
  • Kingunge: Watanzania kuchagua wagombea waaminifu
  • Ofisa Ugavi mbaroni kwa tuhuma za kughushi
  • Askari waadhimisha miaka 46 JWTZ kwa kujitolea damu
  • Bakwata yataka ufafanuzi wa ‘hukumu ya baraghashia’
  • Tigo yaja na Tigo Pesa
  • Ewura yapata mwarobaini wa uchakachuaji mafuta
  • Mfuko wa Pembejeo Wilaya wawa kikwazo kwa wakulima
  • Mbeya kutahini darasa la saba 77,142
  • Ndege yaanguka Rukwa
  • Kikwete azidi kumwaga ahadi
  • Slaa kupunguza posho za wabunge, VAT
  • Mkameruni akamatwa na dola bandia 74
  • Lori lamuua dereva wake
  • Mgombea CUF amuunga mkono Kikwete
  • CUF ikiingia madarakani kupandisha bei ya kahawa
  • Umoja wa Mataifa watoa mafunzo kwa wagombea
  • CUF walia hujuma katika kampeni

  • Habari zinazosomwa zaidi:
  • Balaa lingine kwa Chenge
  • Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
  • Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
  • ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
  • Vatican yamvua jimbo Askofu
  • Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
  • Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
  • Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
  • Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
  • JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
  • Polisi nchini inashirikiana na Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) ili kubaini wahusika wa mtandao wa gazeti tando la zeutamu. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Msemaji wa Polisi, Juma Said Ally, alisema Polisi inashirikiana na Interpol ili kubaini wamiliki wa mtandao huo.

    Alisema wanaamini wahusika wapo ndani na nje ya nchi na hivyo wameamua kushirikiana nao ili kuwakamata na sasa wanaendelea na uchunguzi. “Tunashirikiana na Interpol ili kuwakamata wahusika wanaodhalilisha viongozi na watu mbalimbali na tunaamini wahusika hawa wapo ndani na nje ya nchi, hivyo tunaendelea na uchunguzi,” alisema.

    Hatua hiyo ya Polisi kusaka wahusika wa mtandao huo inakuja baada ya wananchi kukerwa na udhalilishaji unaofanywa na wahusika hao kupitia mtandao huo. Siku za karibuni mtandao huo umekuwa ukitumia nafasi ya uhuru wa vyombo vya habari kudhalilisha viongozi, jambo ambalo ni kinyume na maadili ya jamii na uandishi wa habari.

    Wakati huohuo, wamiliki wa vyombo vya usafiri wa majini na manahodha wa vyombo hivyo, wametakiwa kuwa na vifaa vya uokoaji ambavyo vitasaidia wanapokumbwa na dhoruba baharini au ziwani. Tahadhari hiyo imetolewa kutokana na majanga ya hivi karibuni mkoani Tanga na juzi majahazi mawili kuzama eneo la Kisiju, Pwani.

    Ally alisema jahazi la kwanza liitwalo Dochiwel, lilipigwa na dhoruba na kuzama saa 8 mchana na watu 24 waliokolewa na boti ya Polisi Mv Mamba iliyokuwa ikienda kusaidia uokoaji, ilipata msukosuko baharini na kulazimika kurudi. Aidha, jahazi la Kumekucha lilizama baharini na mizigo iliyokuwa ndani yake saa 12.58 jioni eneo la Mbalukuni, Mafia.

    Jahazi hilo lilikuwa likitoka Dar es Salaam likiendeshwa na Khamis Mohamed (35) likiwa limesheheni mifuko 65 ya ngano, mchele mifuko 15, maharage 43, viroba 80 vya sukari, mabati bandari tano na mbao 15 na mabaharia watano ambao walijiokoa.

    Katika hatua nyingine, Polisi imesema tuhuma za mafisadi alizozitoa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi juzi kudai nchi inahujumiwa na kundi dogo la mafisadi, si mpya kwani baadhi ziko mahakamani na nyingine zipo katika hatua za upelelezi. Ally alimsihi Mengi kama ana jambo jipya aliwasilishe Polisi kwani polisi hawawezi kuzungumzia kesi zilizo mahakamani. Juzi Mengi alizungumza na waandishi wa habari na kuwataja wafanyabiashara watano akidai wameifikisha nchi pabaya na kwamba hawaguswi na serikali.

     
         
     
    Jumla Maoni (4)
         
    Maoni   waachieni jamani ndio uhuru wenyewe jamani, kwani viongozi hawapaswi kuandikwa?
         
    Maoni   haaa mimi mwenyewe nipo nje ya nchi na nilikuwa naifungua zeutamu daily.kweli niliamini binadamu wa siku hizi hawamwogopi mungu licha ya hiyo serikali.duuuh.....
         
    Maoni   kwanza napenda kusema kuhusiana na swala hili la the utamu ni sisi wenyewe tumerisababisha wenyewe wazungu wametuchezea thought wakareta computer kwa hio kuzuia itakuwa ngumu labda hao makachero wapite nyumba hadi nyumba na wasitukizie kiana other wise hawatofanikiwa kwa sababu mwanadamu ana mbinu nyingi leo ukianzia nyuma yeye anapitia mbere
    shukurani kwa sugestions zenu njema.
         
    Maoni   Mmomonyoko wa maadili umefikia mahali pabaya kiasi cha kuiweka rehani heshima na utu wa binadamu, jamani siyo kila kitu kinachofanywa na wazungu ni sahihi , tusiwe watumwa wa mabadiliko,kwa nini tusilinde nidhamu yetu ya kiafrika kuliko kuburutwa na mienendo mibovu ya kimagharibi, inaniuma na kunisikitisha fedha imechukua heshima na utu wa mwanadamu,angalia mfano rahisi kuhusu miziko inayopigwa ya ndombolo , wanawake wanavaa ovyo, mavazi ambayo baba mzazi wa wacheza shoo hao hawezi kukaa na kuangalia miziki hiyo , kisingizio ni utandawazi, nawasihi watanzania wenzangu tuwe na mitazamo sahihi kuhusu utu na heshima ambayo Mungu ametupa, Kuibuka kwa kundi hili dhalimu linalobeza na kubomoa misingi ya utu na heshima iliyowekwa na waasisi wetu wa Taifa (ze utamu) ni matokeo ya kubembeleza na kulea uhuru wa habari usio na tija wala maslahi yoyote kwa taifa,jamani vyombo vya dola tunawamba chonde chonde wasakeni na wadhibitini kwa nguvu zote ili tuliponye Taifa hili Tulilopewa na MUNGU. Mungu awabariki sana.
         
     
     
      Tuma Maoni yako
       

    Jina la Kwanza:

    Jina la mwisho:
    Baruapepe: Barua Pepe imekosewa.
    Maoni yako:   Andika Maoni yako tafadhali.Tafadhali andika Maoni yako.
     
     
     
    WAZO LANGU
    Image

    Magereza fanyieni kazi malalamiko ya wafungwa

    SOMA | HIFADHI
    SAFU
    Image

    Tekuteku za Tefutefu!

    SOMA | HIFADHI
    NYOTA WA WIKI
    Image

    Mtangazaji kajikomboa kwa kuanzisha redio

    SOMA | HIFADHI
    JISAJILI NASI
    Jina la kwanza:
    Jina la Ukoo:
    Baruapepe: A value is required.
     
     
     
    Wasiliana nasi mhariri@habarileo.co.tz, advertising@dailynews.co.tz
    Simu:+255 22 2 127492 au 22 2 116074 au +255 22 2 110595 au 22 2 127493
    HabariLeo © 2009 Haki zote zimehifadhiwa.
    DailyNews Building, Plot 7, Samora Avenue, Box 9033, Dar es Salaam, Tanzania Copyright © 2009 DailyNews Media Group
    Advertisement
    TSN Adveritising