EWURA Banner
HabariLeo Logo
 
Tafuta:
 
 
 
Habari za Michezo na Burudani

Nasma afariki dunia, Khadija Kopa amlilia
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 22nd June 2009 @ 18:01 Imesomwa na watu: 1577; Jumla ya maoni: 0


Habari Zaidi:
  • Taswa FC uwanjani dhidi ya Oryx Oil kesho
  • Kambi ya riadha iko shwari
  • Sheila amtibulia Tatiana BBA
  • Ngasa, Mrwanda waogopwa Algeria
  • Tenisi nao wagomea kama mabondia
  • Mashindano ya Shimiwi 2010 yafutwa
  • Washindi Shinda Mkoko Vodacom wapewa chao
  • KASHFA KARUME BOYS: TFF yaitaka ZFA isikwepe lawama
  • Rage: Siwategemei Friends of Simba
  • Twiga Stars walipwa malimbikizo ya posho
  • JWTZ yawagalagaza wanajeshi wa India
  • Kutolewa Sheila kwaleta mpasuko BBA
  • Kocha: Stars ina uwezo
  • ZFA yaitaja TFF kashfa Karume Boys
  • TGU yazipa changamoto klabu za gofu
  • Busigara bingwa wa mashindano ya Bell
  • Mburahati kusaka mrembo wao Idd mosi
  • Twanga Pepeta yanogesha kampeni Mvomero
  • Simba kutumia Uwanja CCM Kirumba
  • Miss Tanzania watamba wameiva kiutalii

  • Habari zinazosomwa zaidi:
  • Balaa lingine kwa Chenge
  • Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
  • Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
  • ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
  • Vatican yamvua jimbo Askofu
  • Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
  • Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
  • Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
  • Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
  • JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
  • Mwimbaji mahiri wa taarabu nchini, Nasma Khamis 'Kidogo' amefariki dunia. Akizungumza Dar es Salaam jana, baba mdogo wa marehemu, Hamis Kaniki alisema Nasma alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi kutokana na homa ya malaria.

    "Mara kwa mara Nasma alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya moyo, ndio ugonjwa wake mkubwa, lakini miezi ya karibuni alipata nafuu akawa anafanya shughuli zake. "Lakini kuanzia Ijumaa alishikwa na homa ya malaria, ambayo iliibua tena matatizo ya moyo hadi mauti yalipomfika, " alisema Kaniki.

    Alisema hadi mauti yanamkuta Nasma alikuwa akijishughulisha na masuala ya biashara pamoja na mifugo, ingawa pia usanii alikuwa akiendelea lakini akiwa anajitegemea. Alisema Nasma alizaliwa miaka 57 iliyopita Kilwa Kivinje na alibahatika kupata watoto wanane, ambapo sita wapo hai wakati wawili ni marehemu na kuwa maziko yatafanyika leo makaburi ya Kisutu Dar es Salaam.

    Akizungumza kwa simu kutoka Biharamulo jana, mpapasa kinanda wa kundi la TOT Plus, Juma Abdallah 'JJ Mzee wa Mbezi', alisema amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kifo cha Nasma maana yeye ndiye aliyempokea kwenye kundi la Tanzania One Theatre (TOT sasa TOT Plus) mwaka 1993 wakati msanii huyo alipokuwa akitokea Zanzibar.

    "Kama kuna mtu anamfahamu vizuri Nasma, basi mimi ni mmojawao, maana ndiye nilimpokea kutoka Zanzibar alikokuwa akifanya shughuli za muziki, nikamkaribisha TOT na nilifanya naye kazi kwa karibu zaidi," alisema JJ.
    Akiwa TOT, Nasma aliimba nyimbo za Kamba ya Mgomba, Koroboi, Ikwinini na Kidudu Mtu, kisha akajiunga na Kundi la Muungano Cultural Troupe, ambako alishiriki kuimba nyimbo mbalimbali lakini zilizompa umaarufu zaidi ni Kaona Mambo Iko Huku na Sanamu la Michelin. Nasma ambaye pia alipata kuimbia kundi la Babloom Modern ingawa hakung'ara sana, atakumbukwa kutokana na upinzani uliokuwepo miaka ya 1990 kati yake na Khadija Omar Kopa, wakati huo Nasma akiwa Muungano na Khadija akiwa TOT. Wapenzi wa mipasho wanamkumbuka Nasma ambaye alikuwa akiimba mashairi yaliyotungwa na Mustapha Ramadhan wakiwa Muungano, wakishindana na Kopa aliyekuwa akiimba mashairi yaliyotungwa na Othman Soud wote wakiwa TOT. Ilifikia wakati misemo kama Taarab Imo? Au Taarab Anayo, ilikuwa maarufu nchini na ilitokana na nyimbo za mipasho za Nasma na Kopa. Akizungumza jana kutoka Biharamulo ambako kundi la TOT Plus lipo kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Biharamulo Magharibi, Khadija ambaye hujulikana kama Malkia wa mipasho, alisema msiba wa Nasma ni pigo kwa taarabu na ameupokea kwa masikitiko maana alikuwa mtu wake wa karibu. "Alikuwa kama dada yangu, wengi walidhani sisi ni maadui, lakini ukweli ni kuwa tulikuwa wapinzani jukwaani, lakini nje ya jukwaa ni watu wamoja na wenye kuheshimiana. "Kuna matangazo nilipewa nifanye lakini nikawaambia nikiwa na Nasma itapendeza zaidi, sasa kama ingekuwa nina upinzani naye sidhani kama ningemuunganisha kwenye ile kazi. "Jambo la msingi tumuombee mwenzetu Mwenyezi Mungu amuweke mahali pema peponi, maana kifo ni cha kila mtu, wote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea," alisema Khadija. Nasma pia alipata kushirikishwa na kundi la muziki wa kizazi kipya la Gangwe Mobb lililokuwa likiundwa na Haruna Kahena 'Inspekta Haroun' na Kalama Bakari 'Luteni Kalama' katika wimbo Vidonge. Hadi umauti unamkuta alirekodi na kundi la taarab la Super Shine wimbo uitwao Unajishuku, ambao umekuwa maarufu katika vituo mbalimbali vya redio nchini. Mungu amuweke Mahali Pema Peponi.Amin.

     
         
     
    Jumla Maoni (0)
         
     
     
      Tuma Maoni yako
       

    Jina la Kwanza:

    Jina la mwisho:
    Baruapepe: Barua Pepe imekosewa.
    Maoni yako:   Andika Maoni yako tafadhali.Tafadhali andika Maoni yako.
     
     
     
    WAZO LANGU
    Image

    Magereza fanyieni kazi malalamiko ya wafungwa

    SOMA | HIFADHI
    SAFU
    Image

    Tekuteku za Tefutefu!

    SOMA | HIFADHI
    NYOTA WA WIKI
    Image

    Mtangazaji kajikomboa kwa kuanzisha redio

    SOMA | HIFADHI
    JISAJILI NASI
    Jina la kwanza:
    Jina la Ukoo:
    Baruapepe: A value is required.
     
     
     
    Wasiliana nasi mhariri@habarileo.co.tz, advertising@dailynews.co.tz
    Simu:+255 22 2 127492 au 22 2 116074 au +255 22 2 110595 au 22 2 127493
    HabariLeo © 2009 Haki zote zimehifadhiwa.
    DailyNews Building, Plot 7, Samora Avenue, Box 9033, Dar es Salaam, Tanzania Copyright © 2009 DailyNews Media Group
    Advertisement
    TSN Adveritising