EWURA Banner
HabariLeo Logo
 
Tafuta:
 
 
 
Habari za Michezo na Burudani

Mgosi akatwa usajili Simba
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 16th July 2009 @ 08:02 Imesomwa na watu: 961; Jumla ya maoni: 0


Image
Musa Mgosi

Habari Zaidi:
  • Taswa FC uwanjani dhidi ya Oryx Oil kesho
  • Kambi ya riadha iko shwari
  • Sheila amtibulia Tatiana BBA
  • Ngasa, Mrwanda waogopwa Algeria
  • Tenisi nao wagomea kama mabondia
  • Mashindano ya Shimiwi 2010 yafutwa
  • Washindi Shinda Mkoko Vodacom wapewa chao
  • KASHFA KARUME BOYS: TFF yaitaka ZFA isikwepe lawama
  • Rage: Siwategemei Friends of Simba
  • Twiga Stars walipwa malimbikizo ya posho
  • JWTZ yawagalagaza wanajeshi wa India
  • Kutolewa Sheila kwaleta mpasuko BBA
  • Kocha: Stars ina uwezo
  • ZFA yaitaja TFF kashfa Karume Boys
  • TGU yazipa changamoto klabu za gofu
  • Busigara bingwa wa mashindano ya Bell
  • Mburahati kusaka mrembo wao Idd mosi
  • Twanga Pepeta yanogesha kampeni Mvomero
  • Simba kutumia Uwanja CCM Kirumba
  • Miss Tanzania watamba wameiva kiutalii

  • Habari zinazosomwa zaidi:
  • Balaa lingine kwa Chenge
  • Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
  • Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
  • ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
  • Vatican yamvua jimbo Askofu
  • Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
  • Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
  • Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
  • Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
  • JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
  • KLABU ya Simba ya Dar es Salaam imemuengua katika orodha ya wachezaji wake kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao. Habari zilizopatikana ndani ya klabu hiyo jana, zilieleza kuwa jina la Mgosi halipo katika wachezaji waliowasilishwa na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao. Jana ilikuwa mwisho wa timu zote zitakazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kuwasilisha usajili wao Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

    “Leo (jana), ndio mwisho wa klabu kuwasilisha usajili wa wachezaji kwa ajili ya Ligi Kuu msimu ujao na sisi (Simba) tumeengua jina la Mgosi, hayupo katika usajili wetu,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika. Kulingana na chanzo hicho, Mgosi amekatwa kutokana na kuwepo maelezo kwamba anataka kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa Sweden, hivyo uongozi ukaona ni bora aenguliwe.

    Viongozi wa Simba hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, lakini Mgosi mwenyewe alipoulizwa alisema hana taarifa ya jina lake kuenguliwa. “Ndio kwanza nakusikia kwamba nimeenguliwa, pia hata kama ni kweli nataka kwenda nje huwezi kunikata maana nikishindwa majaribio ina maana sina timu.

    “Lakini ngoja nifuatilie nijue kulikoni, ila sina uhakika kama kweli hilo limefanyika,” alisema Mgosi, ingawa chanzo chetu kilituthibitishia kuwa anajua suala la jina lake kukatwa na kwamba mchezaji wa Mtibwa Sugar aliyekuwa amesajiliwa African Lyon kwa ajili ya msimu ujao, Zahoro Pazi ndiye amechukuliwa na Simba kuziba pengo la Mgosi.

    Wakati huo huo, Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Patrick Phiri, aliwasili Dar es Salaam jana na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki na baadhi ya wanachama wa timu hiyo.

    Mashabiki hao wakiongozwa na kikundi cha ushangiliaji cha timu hiyo cha Muchacho maarufu kama Kidedea, walianza kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kuanzia saa saba mchana na waliendelea kuvuta subira uwanjani hapo hadi majira ya alasiri, kocha huyo alipowasili na kuanza kumshangilia kana kwamba ilikuwa mara ya kwanza kufika nchini.

    Akizungumza uwanjani hapo, Phiri raia wa Zambia, alisema amefurahishwa na mapokezi hayo na atawapa mashabiki wa Simba kile wanachokitaka, ambacho ni ushindi kwa timu yao.

    “Sijawahi kupata mapokezi kama haya, nimejisikia furaha sana, nawahakikishia mashabiki wa Simba nitajitahidi kuwapa raha,” alisema Phiri na kuongeza kuwa ana matumaini kikosi kilichosajiliwa kitakuwa imara na kitarudisha heshima ya Simba katika michuano ya ndani na kimataifa.

    Akizungumzia kuhusu kuchelewa kuja nchini, kocha huyo alisema ni kutokana na kuwa na matatizo binafsi na kwamba haikuwa dhamira yake kuchelewa kuja kuinoa timu hiyo. Phiri aliyejiunga Simba mwanzoni mwa duru la pili la Ligi Kuu Tanzania Bara, alienda kwao kwa mapumziko baada ya ligi kumalizika mwezi Aprili na alitarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa mwezi uliopita, lakini alishindwa kufanya hivyo.

     
         
     
    Jumla Maoni (0)
         
     
     
      Tuma Maoni yako
       

    Jina la Kwanza:

    Jina la mwisho:
    Baruapepe: Barua Pepe imekosewa.
    Maoni yako:   Andika Maoni yako tafadhali.Tafadhali andika Maoni yako.
     
     
     
    WAZO LANGU
    Image

    Magereza fanyieni kazi malalamiko ya wafungwa

    SOMA | HIFADHI
    SAFU
    Image

    Tekuteku za Tefutefu!

    SOMA | HIFADHI
    NYOTA WA WIKI
    Image

    Mtangazaji kajikomboa kwa kuanzisha redio

    SOMA | HIFADHI
    JISAJILI NASI
    Jina la kwanza:
    Jina la Ukoo:
    Baruapepe: A value is required.
     
     
     
    Wasiliana nasi mhariri@habarileo.co.tz, advertising@dailynews.co.tz
    Simu:+255 22 2 127492 au 22 2 116074 au +255 22 2 110595 au 22 2 127493
    HabariLeo © 2009 Haki zote zimehifadhiwa.
    DailyNews Building, Plot 7, Samora Avenue, Box 9033, Dar es Salaam, Tanzania Copyright © 2009 DailyNews Media Group
    Advertisement
    TSN Adveritising