Mashabiki Simba, Yanga ‘waalikwa’ kuishangilia JKT Queens

TIMU ya soka ya wanawake JKT Queens inatarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kuwania ubingwa wa majeshi wa dunia kwa wanawake (World Military Women Football Championship) nchini Uholanzi.

Kutokana na jukumu hilo la kitaifa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amewataka mashabiki wa Simba na Yanga kuiunga mkono timu hiyo.

Akiwasilisha makadirio ya mapato ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2023/24 bungeni Dodoma leo Jumatano, Bashungwa amesema mashindano hayo yatafanyika Juni 27 hadi Julai 9, mwaka huu.

“Vilevile, nchi yetu imepata fursa ya kuandaa Mkutano Mkuu wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani ambao utafanyika Jijini Dar es Salaam mwezi Mei 2024,” ameongeza.

Akieleza mafanikio ya timu za Jeshi katika mashindano mbalimbali, Waziri ameliambia Bunge kuwa JKT Queens imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania huku JKT Tanzania iliyokuwa ikishiriki Ligi Daraja la Kwanza imefanikiwa kupanda daraja na msimu wa ligi 2023/24 ambapo Ligi Kuu ya Tanzania Bara

“Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika kuibua vipaji na kuviendeleza kwa lengo la kuinua kiwango cha michezo nchini,” ameongeza.

Habari Zifananazo

Back to top button