loader
Picha

Waziri aitaka Muhimbili kupunguza gharama

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameitaka Bodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kupunguza gharama za matibabu ambazo wananchi wamekuwa wakizilalamikia.

Ummy alitoa maelekezo hayo jana hospitalini hapo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua Maonesho ya Huduma za Afya ikiwa ni sehemu ya maadhimisho Wiki ya Utumishi wa Umma. Alisema malalamiko kuhusu utendaji mbovu wa hospitali hiyo sasa yamepungua isipokuwa yamebaki ya gharama kubwa za matibabu.

Pamoja na kuitaka Bodi ya MNH kuliangalia suala hilo la gharama, aliwaeleza wananchi kuwa suala la matibabu ni la gharama hivyo ili kupata huduma bora bila kupata kikwazo cha fedha ni vema kujiunga na Mifuko ya Bima ya Afya. Alikiri kuridhika na utendaji wa MNH ingawa alisema changamoto ndogondogo kwenye taasisi yoyote hazikosekani mahali popote.

Kwa upande mwingine, alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence Maseru kuweka motisha kwa wafanyakazi ili huduma ziendelee kuwa nzuri zaidi na kuwapa watumishi hao fursa za kuongeza ujuzi na mafunzo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Pia alimtaka kupeleka wataalamu wake wilayani na mikoani ili kujenga uwezo katika vitengo mbalimbali kikiwemo cha wanawake na uzazi. “Katika hili mjipangie mpango kazi kila timu iende kwa wakati wake,” alisema Waziri.

Profesa Maseru alisema katika maadhimisho hayo, Kurugenzi nane za MNH na vitengo vilivyo chini ya Mkurugenzi Mkuu vinashiriki. Profesa Maseru alisema wamejitahidi kuboresha huduma za afya MNH ambapo kwa upande wa figo tangu tangu walipoanza Novemba mwaka jana, wameshawafanyia wagonjwa watano.

Alisema pia mwishoni mwa wiki hii watalaza wagonjwa wengine watano kwa upandikizaji wa figo kama walivyoahidi watakuwa wakifanya hivyo kwa wagonjwa watano kila mwezi. Alisema wanaendelea na maandalizi ya kuanza kutoa huduma mpya za kibingwa nchini ikiwemo upandikizaji wa ini kupitia kitengo cha Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini.

KAMA kawaida ya Watanzania hawawezi kufanya jambo lililotangazwa na serikali ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi