loader
Picha

Pole Mhariri Mtendaji kifo cha Sagati

NAPENDA kukupa pole wewe na waandishi wote wa HabarilLeo na Daily News kwa kuondokewa na mwandishi mahiri;Shadrack Sagati.

Naelewa kwamba ingawaje alishaondoka TSN, lakini hapo ana watu ambao alikaa nao kama familia na ambao wanamjua zaidi kuliko huko alikokuwa kabla ya mauti.

Namkumbuka Sagati tangu tulipokuwa pamoja kwenye fani ya habari, kabla sijaenda kwenye maeneo mengine kitaaluma.

Wakati tunaanzisha HabariLeo, alikuwa mmoja wa timu mahiri anzilishi ambayo ilipewa jina la Real Madrid- wakati huo klabu hiyo ya Uhispania ilikuwa bora Ulaya. Shadrack alikuwa mwandishi mdadisi, aliyejituma kufuatilia vitu.

Alijiamini, kutokana na weledi aliokuwa nao. Alikuwa mahiri kutafuta na kutafiti habari.

Juzi Jumapili nilimuulizia; kwani kuna utafiti ninaofanya kuhusu jambo ambalo nakumbuka Sagati alishaliandikia makala nyingi.

Nikaambiwa yuko Wizara ya Viwanda akiwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano.

Ilikuwa nimtafute Jumanne lakini asubuhi nikakutana na taarifa za kuhuzunisha kwenye mtandao wa Whatsap ambao kuna wadau walioniunganisha. Tumuombee.

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amewasilisha ripoti ...

foto
Mwandishi: Isaac Mruma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi