loader
Picha

Mkandarasi atakiwa akajieleze Dodoma

NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ameagiza Mkurugenzi wa Kampuni ya Nakuroi Investment, Samwel Mollel kwenda Dodoma na kuripoti ofisini kwake kesho Ijumaa saa mbili asubuhi.

Kampuni ya Nakuroi Investment ya Jijini Dar es Salaam ina mkataba wa zaidi ya Sh bilioni 42 kuwasha umeme katika vijiji 111 mkoani Rukwa wa mradi wa usambazaji umeme vijijini (REA III) uliozinduliwa mwaka juzi ambapo hadi sasa ni vijiji vinane tu kati ya vilivyotajwa.

Amewaagiza maofisa sita wanaosimamia REA III Rukwa kupiga kambi Kata ya Mtowisa Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, kuhakikisha umeme unawashwa katika miezi miwili huku akiwakabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dk Halfany Haule.

Amemwagiza Meneja wa Shirika la Umeme mkoani Rukwa (Tanesco), Frank Chambua kuhakikisha wasimamizi hao hawaondoki katika eneo hilo isipokuwa kwa ruhusa ya kimaandishi.

Amewataja wasimamizi hao kuwa ni Meneja wa Tanesco Kanda za Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Salome Mkondola, wasimamizi wa REA III kutoka Dodoma, meneja wa Tanesco Wilaya ya Nkasi, Kalambo na Sumbawanga.

"Nimeagiza Mkurugenzi wa Nakuroia aripoti ofisini kwangu Dodoma kesho (leo), saa mbili asubuhi anieleze kama ameshindwa kazi au kazi zimemzidi apunguziwe.

Ni lazima tupate mwarobaini wa kutekeleza miradi ya REA III mkoani Rukwa hadi kieleweke,”alisema Mgalu. “…Nimeguswa na mateso wanayopata wakazi wa Bonde la Ziwa Rukwa, Sumbawanga kwa kukosa umeme tangu Uhuru. Naagiza umeme uwake ndani ya miezi miwili, " alisisitiza.

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dk Haule alisema atatekeleza maagizo ikiwemo maofisa hao sita kupiga kambi katika Kata ya Mtowisa. Msimamizi wa Nakuroi Investment Company Ltd, Celestine Igongo alimwomba Naibu Waziri Mgalu apatiwe miezi minne ombi lililopingwa.

Rais John Magufuli amemteua Dk. Michael Ng’umbi kuwa Mkurugenzi wa ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi