loader
Picha

Serikali yatimua wanajeshi 67 kwa utovu wa nidhamu

WANAJESHI 67 wa ngazi mbalimbali wamefukuzwa jeshini kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu. Kati yao, 10 ni maofisa wa ngazi za juu huku 57 wakiwa wanajeshi wa vyeo vya kawaida.

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF), Luteni Kanali, Innocent Munyengango alisema wanajeshi hao waliofukuzwa wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali za utovu wa nidhamu.

“Kila mmoja ana tuhuma zake zinazomhusu, lakini zote zina utovu wa nidhamu,” alisema Munyengango Alisema hatua hiyo imechukuliwa kwa mujibu wa sheria za jeshi hilo na kupitishwa na Baraza la Mawaziri lililoongozwa na Rais Paul Kagame.

Kwa mujibu wa Sheria Namba 22/01 ya Oktoba 2, 2016 inaeleza kuwa, askari akifanya jambo lolote la kutia aibu au kudhalilisha, lisilokubalika kwa jamii au linalokwenda kinyume na taratibu za jeshi hilo anastahili kufukuzwa jeshini. Pia ikiwa mwanajeshi amehukumiwa kifungo cha miezi sita anatakiwa kuondolewa jeshini.

WANAFUNZI wa kidato cha sita waliopo katika kambi maalum ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi