loader
Picha

Leseni mpya za udereva kutolewa mwezi huu

MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imetoa ufafanuzi kuhusu ucheleweshwaji wa kutoa leseni za udereva na kusema jambo hilo limesababishwa na mabadiliko ya mfumo wa utoaji leseni ambao hivi sasa unaboreshwa ili leseni ziwe imara na kwamba kazi hiyo itakamilika kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Akizungumza na HabariLeo jana, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema ni kweli kumekuwa na ucheleweshaji wa kupewa leseni kwa madereva walioomba leseni kutokana mfumo wa sasa kubadilishwa. Aliongeza kuwa wataalamu hao wakandarasi wameshafika na wanaendelea kukamilisha kazi hiyo na kwamba ndani ya siku chache kuanzia sasa watakuwa wamemaliza na kuanza kutoa leseni kabla ya mwisho wa mwezi huu.

“Nia ya serikali na TRA ni kuboresha leseni zetu ili ziwe imara na tumekubaliana na Jeshi la Polisi kwa sasa madereva waendelee kutumia leseni za zamani ili mradi tu anaposimamishwa aoneshe risiti ya malipo aliyolipia leseni mpya,” alisema Kayombo. Alisema lengo la kuanzisha mfumo mpya wa kompyuta wa leseni ya kuendesha ni kuisaidia serikali kukusanya taarifa sahihi kuhusu dereva ambazo zitasaidia katika kufuatilia mienendo yao na kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato yake ya kutosha.

Alisema matarajio ya serikali ni kwamba mfumo huo mpya wa kutoa leseni utapunguza ajali za barabarani ambazo nyingi zinasababishwa na madereva ambao hawana sifa za kutosha za kuendesha magari. Kayombo aliwataka madereva ambao wamelipia leseni na hawajazipata kuwa watulivu kwani maboresho hayo yanayofanywa ni katika kuzifanya leseni hizo mpya kuwa imara na kwamba ndani ya wiki mbili kuanzia sasa zitaanza kutolewa. Alisema mfumo mpya wa leseni unachukua nafasi ya mfumo wa zamani ambao hakuweza kutofautisha kati ya aina ya leseni kwa ajili ya kuendesha gari na magari ya abiria ya uwezo tofauti.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi