loader
Picha

RwandAir kupasua anga Italia

SHIRIKA la Ndege la Rwanda `RwandAir’ litazidi kujitanua katika soko la kimataifa kwa kuongeza mdau wa kushirikiana naye katika mambo ya sekta ya anga.

Serikali za Rwanda na Italia zimesaini makubaliano ya ushirikiano wa huduma za anga kwa lengo la kuimarisha biashara ya ndege baina ya nchi hizo.

Kwa makubaliano hayo, ndege za RwandAir sasa zitaweza kutoa huduma Italia huko ndege za Italia nazo zikitoa huduma Rwanda kwa kufuata viwango vya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).

“Hii itasaidia kuboresha mwingiliano wa watu, biashara na utalii kati ya nchi hizi mbili rafiki pamoja na kuleta ushindani wa kibiashara kwa usafiri wa anga kwa nchi husika, ”amesema Waziri wa Miundombinu, Balozi Claver Gatete.

Balozi wa Italia nchini Rwanda, Domenico Fornara alibainisha kuwa nakala walizosaini ni za kisheria ikifuatiwa na masuala ya kiteknolojia bila kuhusisha taasisi za kisiasa.

Kwa sasa RwandAir inafanya safari mbili kwenda Ulaya ambazo ni Kigali-London (Uingereza) na Kigali-Brussels (Ubelgiji), hivyo mkataba huo utafanya shirika hilo la ndege kuongeza huduma zake katika bara la Ulaya.

WACHIMBAJI wadogo wa dhahabu katika mgodi mpya wa Ndurutu, Kijiji ...

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi