loader
Picha

Mtoto wa Lowassa amkubali Magufuli

KAMPENI za Ubunge katika Jimbo la Monduli mkoani Arusha zimeendelea kupamba moto baada ya wagombea wa vyama mbalimbali na wapambe kupishana majukwaani kila upande ukivutia wananchi wauchague.

Mjumbe wa Baraza Kuu la vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Fredy Lowassa jana aliongeza nguvu ya kampeni hizo kwa kumnadi mgombea wa chama hicho, Yonas Laizer huku akikiri hadharani kukubali utendaji wa Rais John Magufuli.

Fredy Lowassa ambaye ni mtoto wa Edward Lowassa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu kabla ya kujiuzulu amesema katika kampeni kata ya Makuyuni kuwa unaweza kuwa upinzani lakini ukaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli na serikali yake jinsi inavyofanya kazi vizuri ya kuwatumikia wananchi.

Amesema huku akishangiliwa na wananchi walifurika katika kata hiyo kuwa hoja ya kuhama upinzani na kujiunga na CCM kwa sababu ya jitihada za Rais Magufuli haoni kama zina mashiko.

Mjumbe huyo alisema kuwa wanaohama upinzani na kubeza upinzani na kutoa sababu za kuunga mkono serikali ya Rais Magufuli wanaweza kuwa na sababu, lakini ingekuwa busara zaidi wakiwa upinzani na kuamua kusema hayo lakini sio kuhama.

''Mimi niko upinzani lakini ninamkubali Rais kwa utendaji kazi wake wa kuwatumikia wananchi hilo halina ubishi lakini kuhama na kujiunga CCM na kutoa sababu hizo sioni kama ni sawa,'' amesema.

Mapema mwaka huu, Lowassa alikwenda Ikulu kumwona Rais Magufuli na kumsifu kwa utendaji kazi wake wa kuwatumikia wananchi hususani katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Fredy mbali ya hilo aliwataka Julius Kalanga, Mbunge wa zamani wa chama hicho aliyehamia CCM na sasa kuteuliwa kuwa mgombea wa chama hicho na diwani wa Monduli Mjini, Isack Joseph maarufu kwa jinala Kadogoo kufanya kampeni za kistarabu na kuacha mara moja kumchafua baba yake.

Alisema wanasiasa hao anawafahamu vizuri sana ni vijana aliowashika mikono na kuwapeleka kwa baba yake na katika kuchangia kufika walipofika baba yake ana mchango mkubwa sana na lazima wawe na fadhila.

Amesema kuna siasa na baada ya siasa na kuendelea kumchafua baba yake wakati ndio aliowapandisha pale walipo ni kumkosea adabu kwa kiasi kikubwa sana na ikibidi atajibu mapigo lakini kwa sasa ametoa onyo.

Akimnadi mgombea wa ubunge wa jimbo hilo Laizer, alisema kuwa ni mgombea ubunge mwenye kujitambua kijana mwelewa sana na yuko tayari kuwatumikia wakazi wa Monduli, hivyo aliwataka wakazi wa Monduli kumchagua mgombea huyo.

Laizer amesema, yeye ni mgombea safi na mwenye sifa za kustahili kuwa mbunge wa Monduli na aliwaomba wananchi wa Monduli kumchagua yeye kuwa mbunge wa jimbo hilo.

SERIKALI inatarajia kupata Dola za Marekani milioni 500 (zaidi ya ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Monduli

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi