loader
Picha

Benki EAC kimataifa zaidi

BENKI nyingi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki zimetanua huduma zake ndani na nje ya jumuiya hiyo katika kutafuta masoko mapya, ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma katika soko la sasa ndani ya jumuiya hiyo.

Kutokana na vita ya muda mrefu ilivyoibuka mara tu baada ya kujipatia uhuru wake mwaka 2011, Sudan Kusini ni taifa pekee ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambalo benki zake zimeshindwa kufanya kazi kutokana na mgogoro huo.

Kutokana na hali hiyo, Sudan Kusini inategemea huduma za kibenki kutoka nje ya nchi za Afrika Mashariki baada ya benki za nchi hizo kushindwa kufanya kazi katika mazingira magumu.

Na kutokana na kushindwa kufanya shughuli zao katika nchi hiyo changa kabisa duniani, benki kubwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeamua kutafuta masoko mapya katika mataifa kama ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Malawi, Burundi na Botswana.

Nchini Tanzania matumizi ya teknolojia ya kidijiti katika shughuli za kibenki zimeifanya Benki ya CRDB kuwa benki bora katika ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na utoaji wa huduma mahali popote katika bara la Afrika na duniani kwa ujumla.

Benki hiyo inatumia utaratibu wa kufanya mambo ya kibenki kidijiti ambao ni utaratibu unaotumiwa na benki nyingi duniani.

Benki hii inatoa huduma nyingi kwa kutumia njia ya kidijiti kuwafikia wateja wake katika kanda nzima ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika. Kwa mfano, benki hii ina huduma ya intaneti inayowezesha kampuni popote pale Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla kuweza kupata huduma za kibenki kwa kutumia Extromet.

Kupitia huduma hiyo, kampuni zinaweza kulipa mishahara ya wafanyakazi wao na kuhamisha na kusafirisha fedha na kufanya karibia kila kitu cha kibenki popote yalipo bila kulazimika kwenda kufungua tawi katika nchi fulani.

Benki ya CRDB iliibuka mshindi wa tuzo ya Benki Bora ukanda wa Afrika Mashariki katika Tuzo za benki bora Afrika “African Banker Awards” 2018 zinazoandaliwa na kampuni ya kimataifa ya uchapishaji ya IC Publications kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB).

Katika tuzo hizi mashuhuri Afrika, Benki ya CRDB ilitunukiwa tuzo hiyo kutokana na matokeo mazuri ya Benki hiyo katika kufikia wateja wapya, ubunifu katika kutoa huduma, matumizi ya teknolojia za kisasa na mchango mkubwa unaotolewa na Benki ya CRDB katika kukuza sekta ya benki na fedha katika Kanda ya Afrika Mashariki.

Nchini Kenya ripoti ya Benki Kuu ya nchi hiyo imeonesha kuwa benki tisa za Kenya zimejitanua zaidi nje ya nchi hiyo kutoka kuwa na matawi 297 mwaka 2016 hadi kufikia matawi 306 mwaka jana.

Kenya ilifanikiwa kufungua matawi 40 ya benki nchini Sudan Kusini lakini kutokana na ukosefu wa usalama yamepungua hadi kufikia 20 ambapo asilimia kubwa ya matawi hayo yaliyobaki yamefungwa.

Kati ya matawi hayo 20, Benki ya Biashara ya Kenya (KCB) ina matawi 11 wakati benki ya Co-operative ina matawi manne na Equity ina matawi matano. Benki hizo sasa zimepeleka huduma zake katika mataifa ya DRC, Burundi, Malawi na Botswana. Mpaka sasa Equity Bank imewekeza nchini DRC na sasa ina matawi 39 kutoka matawi 31 ya mwaka jana.

WACHIMBAJI wadogo wa dhahabu katika mgodi mpya wa Ndurutu, Kijiji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi