loader
Picha

TAHARIRI: Mkutano wa vijana uje na suluhu kero zinazowakabili

ILI kuwa na taifa lenye uhakika na nguvu kazi yake, kitu muhimu ni kutambua matatizo yanayokabili nguvu kazi iliyopo na inayokuja. Tunasema hivyo, kwa kuwa taifa lolote lile lisiloangalia changamoto za nguvu kazi zake, ipo hatari likaingia katika umaskini usioweza kubadilishwa kirahisi.

Taifa hilo kwa hakika litaingia katika umaskini kwa kuwa litalazimika kutafuta nguvu kazi na kuilipia kitu, ambacho kitaleta shida kubwa katika uendelezaji wa teknolojia na kulinda mafanikio yaliyokwishapatikana katika nyanja mbalimbali.

Kwa kuwa taifa hili limejikita katika kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda, ni lazima kuangalia namna ambavyo tunashughulikia kundi hili la wazalishaji, ambalo kwa sasa lina mitafaruku mingi ikiwamo lishe, afya na uduni wa huduma zenye elimu rika. Kutokana na ukweli huo, tunapongeza mkutano wa siku tatu unaofanyika Dodoma, ambao unazungumzia changamoto za vijana balehe katika afya na ustawi, tukitegemea kwamba hata suala la dawa za kulevya litazungumzwa na kuwekewa mikakati kukabiliana nalo.

Vijana hawa wakiwa katika hali bora, ndio msingi mkubwa wa nguvukazi ya taifa hili, kwani wao ndio watakaokuwa na uwezo wa kuendeleza kizazi na pia kuambukiza teknolojia.

Tunasema hayo kwa kuwa tayari imeelezwa kuwa kuwa theluthi moja ya vijana wamekosa lishe huku asilimia 27 wakiwa na tatizo la upungufu wa damu, jambo ambalo linatarisha nguvu kazi ya Taifa. Kama takwimu zilizopo zilizoelezwa katika mkutano huo, kwamba vijana ambao ni asilimia 10 ya Watanzania, wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi ambazo zinakwamisha makuzi hayo, ipo haja ya kutafuta suluhu, kwani hiyo ndiyo nguvu kazi inayotarajiwa kuupa uhai mchakato wa maendeleo ya nchi.

Kwa sasa vijana wetu wanapokabiliwa na changamoto hizo, watendaji serikalini wanatakiwa kuwasaidia wananchi kutambua umuhimu wa kubadilika na kuangalia afya ya watoto kwa kudhibiti ukatili na pia kuwapa lishe inayofungua bongo zao.

Katika kuangalia mustakabali wa vijana, mkutano huo unaofanyika wakati asilimia 63 ya vyoo katika shule si rafiki kwa mtoto wa kike huku asilimia 40 ya vijana wanashindwa kuendeleza na masomo ya sekondari, unatakiwa kuja na azimio linalotoa mpangilio wa kukabiliana na matatizo ili nguvu kazi yetu isiathirike. T

unataka kuamini kwamba nguvu kazi hii ikilindwa na kutatuliwa changamoto zake, itawezesha nchi kuwa na uhakika na taifa la kesho.

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi