loader
Picha

Yanga yaipasua African Lyon

BAO moja lilofungwa na mshambuliaji, Yusuph Muhilu limetosha kuipa Yanga ushindi katika mchezo wa kirafi ki dhidi ya African Lyon.

Mhilu aliyeingia kuchukua nafasi ya Mrisho Ngassa alifunga bao hilo pekee katika dakika ya 84 baada ya kazi nzuri aliyofanywa na matheo Antony.

Katika mchezo huo ulipigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam timu zote zilifanya mashambulizi kadhaa lakini hayakuwa na faida kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko kadhaa kwa kuwatoa Mrisho Ngassa, Deus Kaseke, Pius Buswita, Raphael Daudi, Heritier Makambo na kuwaingiza Ibrahimu Ajib, Matheo Anthony, Papy Tshishimbi. Mhilu. Jaffar Mohamedi na Amis Tambwe.

Baada ya mabadiliko hayo Yanga ilionekana kuonana na kufanikiwa kupata bao hilo la pekee lililofungwa na Mhilu kwa kichwa.

Kivutio kwenye mchezo huo alikuwa kiungo mshambuliaji Haruna Moshi’Boban’ ambae alionyesha uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kutengeneza nafasi kadhaa za mabao ambazo washambuliaji wa African Lyon walishindwa kuzitumia.

WAKATI Klabu ya Simba wakidhamiria kumpeleka mwanachama wa timu hiyo ...

foto
Mwandishi: Mohammed Mdose

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi