loader
Picha

Wema kuzindua filamu mpya

BAADA ya ukimya wa muda mrefu Malkia wa fi lamu nchini Wema Sepetu ametangaza ujio wa matukio mawili kwa mpigo.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Instagram, Wema alitaja ujio wa filamu yake mpya ya ‘Dad’ alioshirikiana na Van Vicker kutoka Nigeria pamoja na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

“The Moment tuliokuwa tukisubiria sana sio, I hope you are Ready (mko tayari),” aliandika Wema. Wema alisema matukio hayo yatafanyika katika ukumbi wa Mlimani City kwa kiingilio cha Tsh 50,000 O ktoba 28 mwaka huu.

Tangu kuanza kwa mwaka huu, Wema ambaye pia ni Miss Tanzania 2006 amekuwa akitangaza tukio hilo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, ambapo wadau wake wengi hawakufahamu alichokuwa akimaanisha.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Simba leo ...

foto
Mwandishi: Rahim Fadhili

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi