loader
Picha

Kigwangalla aruhusiwa kutoka Muhimbili

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla ameruhusiwa kutoka Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) alikokuwa amelazwa akimshukuru Mungu kuwa ameokoka katika ajali ambayo wetu wengi walitegemea kuwa angekufa. Dk Kigwangalla alitoka katika jengo la hospitali hiyo jana baada ya madaktari kujiridhisha kuwa afya yake imetengamaa na anaweza kurejea nyumbani.

Akizungumzia ajali hiyo, Waziri Kigwangalla alisema ilikuwa ni mbaya sana na kuwa kupona kwake ni mpango wa Mungu na jitihada za madaktari na wahudumu wa afya waliompokea na kumhudumia. “Mungu amenibariki sikufa kwa ajali ile, kila mtu alitegemea ningekufa, ni jitihada pia kubwa za wahudumu wa afya walionipokea kutoka kituo cha afya kule Magugu na matibabu niliyopata kwenye helikopta,” alisema Dk Kigwangalla.

Agosti 4, mwaka huu, gari aliyokuwa amepanda waziri huyo ilipata ajali katika kijiji cha Magugu mkoani Manyara na kusababisha kifo cha Ofisa Habari wa wizara hiyo, Hamza Temba wakiwa safarini kuelekea mkoani Dodoma. Dk Kigwangalla aliwashukuru wahudumu wa afya, ikiwa ni pamoja na madaktari katika hospitali ambazo alipatiwa matibabu baada ya kupata ajali hiyo ambayo alisema anaamini kwa kiasi kikubwa walichangia uponaji wake. Alisema pamoja na kwamba ameruhusiwa kutoka hospitali hapo, lakini tiba yake haijakamilika kwani mkono haujanyooka vizuri na kuwa atahitajika kutolewa pini aliyowekewa kwenye mkono kama sehemu ya matibabu na kisha kuendelea na mazoezi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na ...

foto
Mwandishi: Regina Mpogolo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi