loader
Picha

Waliopisha Ikulu Chamwino walipwa mabilioni

SERI KALI imeanza kuwalipa fi dia wananchi waliopisha ujenzi wa Ikulu ya Chamwino, kupisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma pamoja na uwekeji taa katika uwanja huo. Ulipaji fidia huo ulielezwa jana mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge na Mkurugenzi wa Miliki wa Wakala wa Majengo (TBA), Baltazar Kimangano na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya V iwanja vya Ndege (TAA), R ichard Mayongele.

Mkurugenzi Miliki wa TBA, Kimangano alisema Sh bilioni 7 za kulipa fidia wananchi waliopisha ujenzi wa Ikulu zimetolewa na R ais John Magufuli ambapo kati yake, Sh bilioni 5.3. zimetolewa jana kwa wananchi 2,005 waliohakikiwa. “Baada ya kufanya uhakiki tumebaini kwamba wananchi 2,005 kati ya 2,716, wanatakiwa kulipwa na jana tumeanza kuwalipa fedha zao,” alisema Kimangano na kuongeza: “Wananchi 714 waliobaki watahakikiwa na mara uhakiki ukikamilika watalipwa kwa sababu fedha zipo na serikali imetoa fedha hizo kwa ajili ya kuwalipa wananchi hao.”

Alisema wananchi wanaohusika ni waliopo katika eneo la ekari 8,473 zilizochukuwa kutoka kwa wananchi 3,191 waliopo katika “V ijiji vya Bwigiri, Kalama, Malecela, Mwongozo katika wilaya ya Chamwino na kwa upande wa Jiji la Dodoma ni vijiji vya V ikonze na Chamvu katika mtaa wa Muungano. Alisema utaratibu wa kulipa ulianza mwezi Desemba na Januari kwa wananchi 472, wakabaini kwamba wengine walioingia kutaka kulipwa walikuwa si wamiliki halali wa maeneo hayo.

Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mayongele alisema mamlaka hiyo imetenga jumla ya jumla ya Sh bilioni 13 kutokana na mapato ya ndani kutokana na tathmini iliyofanywa mwaka 2016 iliyolenga kuongeza meta 530 kwa ajili ya kuweka taa za kuongozea ndege. Mayongele alisema katika awamu hii inawalipa fidia wananchi 60 waliopo katika eneo la mita 150, na hivyo litabaki eneo la mita 330 ambalo itaendelea kulipa fidia hapo baadaye. “Wananchi hao watalipwa fidia ya Sh bilioni 3.392 katika mtaa wa Chadulu B ili kuboresha uwanja wa ndege wa Dodoma ili uweze kufanya kazi kwa saa 24 kwa siku,” alisema.

Alisema awali mamlaka hiyo ilitoa fidia kwa wananchi waliopo katika meta 50 za kwanza kwa kutoa Sh bilioni 2.1, na sasa katika awamu ya pili inawalipa wananch hao 60. Mamlaka hiyo itaendelea kulipa kidogo kidogo ili lengo la kufikia meta zote 530 zinafikiwa ili uwanja huo uwe katika kiwango bora kwa kupokea ndege kwa saa 24 wakati wa mchana na usiku.

Akihitimisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Mahenge, alisema wakati anaingia katika mkoa huo Novemba mwaka jana, alikuta mezani kwake migogoro miwili ya fidia inayohusu kupisha ujenzi wa Ikulu na kupanua uwanja wa ndege. “Nafurahi kwamba watendaji hawa wawili wamefikia hatua ya kulipa fidia kwa wananchi ambao wamepisha maeneo mawili hayo kuendelezwa kujenga,” alisema.

WANAFUNZI wa kidato cha sita waliopo katika kambi maalum ya ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi