loader
Picha

Auawa kwa kupigwa risasi kwa kuvamia kambi ya JWTZ

MTU mmoja mwanaume ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja amekufa kutokana na kuvuja damu nyingi baada ya kujeruhiwa kwa risasi alipojaribu kukimbia na kukaidi amri ya kusimama alipoingia kwenye kambi ya jeshi kinyume cha utaratibu. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, mtu huyo aliingia kwenye Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) kwenye kambi iitwayo Mapinga Comprehensive Training Centre (CTC).

Nyigesa alisema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 11, saa 9 alfajiri kwenye kambi hiyo iliyopo Mapinga wilaya ya Bagamoyo ambapo aliingia kwa kuruka ukuta. “Mwanamume huyo baada ya kuingia, walinzi wa JWTZ ambao walikuwa zamu walimwamuru asimame lakini aliendelea kukimbia pia walirusha risasi hewani ili asimame lakini alikaidi na kuzidi kukimbia ndipo walimfyatulia risasi iliyompata kiunoni,” alisema Nyigesa.

Alisema kuwa baada ya kufyatuliwa risasi hiyo alidondoka chini na kuanza kuvuja damu na alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitali kutokana na damu nyingi kuvuja. “Tunatoa mwito kwa wananchi kuacha kuingia kwenye maeneo ya jeshi na yale ya hifadhi yenye ulinzi wa askari pasipo kufuata taratibu za kisheria ya kuingia kwenye maeneo hayo,” alisema Nyigesa.

Aidha alitoa rai kwa wananchi pale wanapokuwa wameingia kwenye maeneo hayo ni vema kuwa watiifu wanapotakiwa kusimama ili kuweza kuhojiwa na kuelekezwa iwapo watakuwa wameingia kwenye maeneo hayo kimakosa. “Ifahamike kuwa maeneo yote yenye ulinzi wa askari yana taratibu zake ambazo zinapaswa kuheshimiwa na kila mmoja wetu jambo ambalo mtu huyo angekuwa amezifuata taratibu hizo basi pasingeweza kutokea madhara hayo,” alisema Nyigesa.

WANAFUNZI wa kidato cha sita waliopo katika kambi maalum ya ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi