loader
Picha

Try Again awatoa wasiwasi Simba

KAIMU Rai s wa Simba, Salim Abdallah ‘T ry Again’ amewatoa wasiwasi wanachama wa klabu hiyo baada ya kutochukua fomu ya kugombea uongozi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao. Simba ipo kwenye mchakato wa kufanya uchaguzi wa kwanza baada ya kubadilisha mfumo wa uendeshaji kuwa wa hisa, na Try Again alitarajiwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo anayoikaimu kwa zaidi ya mwaka sasa.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Try Again alisema bado yupo ndani ya klabu hiyo na atashirikiana kwa karibu na viongozi watakaochaguliwa kwa kuwapa ushauri na kusimamia mambo mbalimbali akiwa nje ya uongozi. “Kwa sasa Simba aihitaji kujadili mtu, kwani kiongozi wa Simba sio mtu bali ni bodi kwa maana tunazungumzia kampuni,” alisema Try Again. “Unapozungumzia kampuni haimaanishi ni mtu fulani… “ Kampuni na mwenye kampuni ni vitu viwili tofauti kwa hiyo niwatoe hofu wanasimba wasiwe na wasiwasi Simba iko salama na imara na mimi kama mwanachama nitaendelea kubaki kiongozi kwa kushauri na kuonesha njia kwa uzoefu wangu nilioupata kidogo kuhakikisha Simba inaendelea kufanya vizuri,” aliongeza.

Alisema, asingependa kutafsiriwa mafanikio yake ndani ya Simba yametokana na kujiwekea mizizi ya kudumu ndani ya klabu hiyo. “Nisingependa mafanikio yangu niliyoyapata ndani ya kipindi kifupi niliyoongoza Simba kuwa najitengenezea njia ya kuwa kiongozi wa kudumu.” “Nikiwa chini ya uongozi wangu nikiwa nakaimu nafasi ya urais nimesimamia mabadiliko kutoka mfumo wa wanachama kwenda mfumo wa hisa… .,” alisema.

“Nimefanikisha mchakato huo na sasa Simba ipo kwenye mfumo mpya inatosha, nikigombea uongozi ndani ya Simba kutakuwa na mgongano wa kimaslahi… “Wakati naingia kwenye uongozi kwa muda mrefu Simba ilikuwa haijashinda ubingwa wa ligi Tanzania. Nashukuru niliweza kuiongoza kushinda ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara. “Endapo nitagombea inaweza kutafsiriwa kuwa nilifanya hivyo nikiwa najitengenezea mazingira ya kuja kuongoza baadae,” alisema.

Alisema muundo wa Simba kwa sasa sio wa kuongozwa na mtu mmoja kama ilivyo sasa unaomaliza muda wake, sasa ni kampuni yenye bodi ya wakurugenzi, wahasibu kwa hiyo hao wote wataiongoza Simba kwa ufanisi. Wanachama waliochukua fomu kugombea nafasi mbalimbali ni 21 ambapo wanaogombea uenyekiti ni, wawili wa Ujumbe kwa Wanawake na 17 kwa Wajumbe wa Bodi. Katika nafasi ya Mwenyekiti wagombea ni mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Mtemi R amadhani Swedi Nkwabi. Nafasi za Wajumbe wa Wanawake waliojitokeza ni Jasmin Soud anayetetea nafasi yake na Asha Baraka wakati wajumbe wa Bodi ni Hussein Mlinga, Iddi Kajuna, Dk. Zawadi Kadunda, Mohammed Wandi, Suleiman Said, Abdallah Mgomba na Christopher Mwansasu.

Wengine ni Alfred Elia, Mwina Kaduguda, Ally Suru, Said Tully, Juma Pinto, Hamisi Mkoma, Abubakar Zebo, Omar Mazola, Patrick R weyemamu na Suleiman Suleiman. Mwisho wa kurudisha fomu ni Jumamosi wiki hii, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam. Katiba mpya ya Simba inaelekeza Mwenyekiti wa klabu awe na elimu ya Shahada ambaye ataongoza Bodi ya Wakurugenzi itakayokuwa na wajumbe wanane chini yake. Na mwenyekiti huyo atakuwa na mamlaka ya kuteua wajumbe wengine wanne, kati yao mmoja lazima awe mwanamke ili kukamilisha Bodi ya wakurugenzi ya watu wanane.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi