loader
Picha

Mtibwa hawachomoki -Matola

KOCHA wa Lipuli, Selemani Matola ameivaa Mtibwa Sugar na kueleza kuwa anaifahamu ilivyo ngumu kucheza nayo kutokana na ubora walionao, lakini hilo siyo tatizo kwao kutokana na walivyojipanga kuwashushia kipigo. Miongoni mwa mambo yanayomuaminisha Matola kuibuka na pointi tatu katika mchezo huo utakaopigwa Jumamosi hii katika uwanja wao wa nyumbani wa Samora uliopo Iringa. Matola aliliambia gazeti hili kuwa Mtibwa si timu ya kubeza na ndiyo maana wapo kwenye maandalizi kuhusu mchezo huo kwa muda mrefu sasa wakiji panga vya kutosha kuhakikisha wanabaki na pointi tatu baada ya kumalizika kwa dakika 90 siku hiyo.

“Kila mmoja anafahamu Mtibwa ni timu ngumu na timu yenye upinzani mkubwa katika ligi, lakini pamoja na yote hayo sisi tumejipanga kwelikweli kuhakikisha kwamba tunapata matokeo na kuondoka na pointi zote tatu katika uwanja wetu wa nyumbani. “Tumesikia kuwa hawataki kupoteza mchezo kutokana na kujipanga na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na ni kweli siyo wao tu, hata wale ambao hawashiriki Afrika nao wanataka pointi, sasa kwa kuwa sisi tunalifahamu hilo, tutajua nini cha kufanya kutokana na upana wa kikosi chetu ili tupate matokeo,” alisema Matola.

L ipuli imeanza kushiriki L igi Kuu msimu uliopita baada ya kupanda daraja, ilipokutana na Mtibwa kwenye Uwanja wa Samora, ilifungwa kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Hassan Dilunga anayekipiga Simba kwa sasa. L akini pia katika mchezo wa pili wa marudiano uliopigwa Uwanja wa Manungu Morogoro, Mtibwa ilikubali kipigo cha mabao 2-1.

WAKATI Klabu ya Simba wakidhamiria kumpeleka mwanachama wa timu hiyo ...

foto
Mwandishi: Hans Mloli

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi