loader
Picha

Serikali kujenga kambi JKT, kuanzisha miradi

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imelieleza Bunge kuwa, inaanzisha kambi mpya za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika maeneo mbalimbali kwa awamu.

Waziri wa wizara hiyo, Dk. Hussein Mwinyi amesema, Serikali inatambua hitaji kubwa la kuanzisha kambi za JKT kwenye mikoa na wilaya zisizo na kambi hizo.

"Jeshi la Kujenga Taifa limeelekeza nguvu kwenye vikosi ambavyo vilivyoanzishwa awali na baadaye kusitisha shughuli za kuchukua vijana mwaka 1994" amesema Dk. Mwinyi.

Wabunge wameelezwa kwamba, hivi sasa JKT imejikita katika kutoa mafunzo ya stadi za kazi kwa vijana walkiojiunga na jeshi hilo kwa kujitolea.

"Lengo ni kuwa endapo vijana hawa watakosa ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama waweze kuajiriwa na taasisi nyingine za Serikali, sekta binafsi au wajiajiri wenyewe" amesema.

Waziri Mwinyi ameyasema hayo wakati anajibu swali la Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Oscar Mukasa.

Amesema, vijana wanaopata fursa ya kujiunga na JKT kwa kujitolea ni wachache kulinganisha na mahitaji ameahidi kulifanyia kazi wazo la Mbunge huyo kuanzisha miradi isiyohitaji uwekezaji mkubwa na kuwashirikisha vijana wasio na ajira kwenye maeneo yasiyo na  kambi za JKT.

WANAFUNZI wa kidato cha sita waliopo katika kambi maalum ya ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi