loader
Picha

JPM anavyofuata nyayo za Nyerere CCM

R AIS John Magufuli juzi alimaliza ziara ya kikazi ya siku 10 katika mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu alikoweka mawe ya msingi na kuzindua miradi kadhaa ya maji, barabara, hospitali na shule. Alianza ziara hiyo mjini Mwanza kwenye mradi wa ukarabati wa meli za Mv V ictoria na Mv Serengeti na uundaji wa chelezo na meli kubwa ya kubeba abiria 1,200 itakayochukua nafasi ya Mv Bukoba iliyozama na kuua abiria mwaka 1996 katika Ziwa V ictoria ikitokea Bukoba kupitia Bandari ya Kemondo.

R ais anamaliza ziara yake mkoani Singida kwa kuzindua ujenzi wa daraja la mto Sibiti lenye urefu wa takribani mita 80; pamoja na kilomita 25 za kipande cha barabara ya lami mpakani mwa Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu na wilayani Mkalama mkoani Singida. Anaagiza daraja hilo lijengwe usiku na mchana ili likamilike ifikapo Machi 2019. Kabla ya kumaliza ziara yake mkoani Simiyu alikozindua majengo ya wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu na mradi wa ujenzi wa vituo zaidi ya 30 vya afya vilivyojengwa kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), alitokea wilayani Tarime, Mara.

Anaenda Mara akitokea wilayani Ukerewe mkoani Mwanza alikozindua mradi wa maji safi na salama na ujenzi wa barabara ya lami ya kilomita 151 kutoka Bulamba – Kisorya- Nansio kwa wananchi wa huko kabla ya kuingia Bunda na kuagiza kukamilishwa kwa mradi mkubwa wa maji uliokwama miaka mingi. Anaweka pia mawe ya msingi na kuzindua miradi kadhaa ikiwemo ya ujenzi wa Barabara ya Makutano Wilaya ya Musoma Mjini, Musoma V ijijini na Butiama alikozaliwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere akiagiza kuenziwa kwa mwasisi huyo wa chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akiwa na mjane wa Nyerere, Mama Maria, R ais Magufuli anazindua ujenzi wa Barabara ya Makutano na kutembelea Shule ya Msingi Mwisenge mjini Musoma aliposoma Mwalimu Nyerere. Hapo, R ais anaonesha kukerwa na viongozi kutoijali na kuipa umuhimu kama sehemu ya historia ya ukombozi wa nchi hii. Kuonesha anavyoguswa na historia na mchango mkubwa wa Mwalimu Nyerere, R ais Magufuli anatoa fedha kwa ajili ya shule hiyo ili ikarabatiwe na kufanana na jina na historia ya Nyerere huku akiagiza Uwanja wa Ndege wa Musoma kuwekwa lami ili ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL ) zianze kuenda huko.

Kwa jumla, ujumbe mkubwa wa R ais Magufuli akiwa Butiama na mkoa mzima wa Mara ulikuwa ni haja ya watu wa mkoa huo na Watanzania kwa jumla kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo kwa kuienzi amani, umoja, maendeleo, kupinga ufisadi kama moja ya tunu ambazo alizisimamia alipokuwa hai. Anawaonya wananchi wa Mara dhidi ya ukabila na madhara yake akirejea nchi zisizokalika kutokana na watu wake kupigana vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa kuendekeza ukabila.

R ais anarudia kauli ya kumuenzi Nyerere kwa wa- nanchi wa Sigiti akisema chama pekee kinachosimamia hayo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ninafuatilia ziara ya R ais Magufuli mwanzo hadi mwisho na lazima nikiri kuwa, ilikuwa ya mafanikio makubwa na majibu dhahiri kwa utafiti wa taasisi ya Twaweza kuhusu kushuka kwa umaarufu wake (kama kweli utafiti wao ulikuwa sahihi) kwani maelfu kwa maelfu ya watu walijitokeza kumlaki kote. Pengine Twaweza watakuwa wamejifunza kitu kuhusu tafiti zao na uhalisia wake kwa walengwa wa maswali yao kwani umati wa watu maskini kwa matajiri waliojitokeza kumlaki, kumsikiliza na pia kumwombea afya njema na maisha marefu na alindwe dhidi ya mahasidi unaonesha anavyokubalika.

Ili kujua ni kwanini wananchi wanampenda na kumkubali hivyo, R ais Magufuli, mtu hahitaji kuhangaika kufanya utafiti. R ejea tu mambo aliyoyafanya alipokuwa ziarani Mwanza, Mara na Simiyu na shauku waliyokuwa nayo wananchi maelfu kwa maelfu waliojitokeza kumlaki na hata kila alipopita. Kwa kifupi, R ais Magufuli amejipambanua kama kiongozi anayetembea katika nyayo za Mwalimu Nyerere, aliyekuja kutimiza maono na ndoto zake na kuthibitisha kuwa, hazikuwa ndoto tu, bali ukweli. Kwa miaka miwili na nusu aliyokaa madarakani, R ais Magufuli amethibitisha Nyerere alikuwa kama nabii.

Hii ni kwa sababu aliyotamani yafanyike, aliyoyasema, kuwaza kwa ajili ya nchi yake, yanatimia kupitia kwake, mwenyewe akiwa pia tunda la maono hayo ya Nyerere ambaye Kanisa Katoliki alilokuwa muumini wake, limeanzisha na linaendelea na mchakato wa kumtangaza kuwa mtakatifu. Sina hakika kama kukamilika kwa maono ya Nyerere kutasaidia kutangazwa kwake na Kanisa kuwa Mtakatifu kwani mambo hayo yatakuwa ni ushahidi wa miujiza inayosubiriwa kwa hamu itokee ndio watu waamini kweli Nyerere hakuwa kiongozi tu wa kawaida ndani na nje ya nchi, bali alikuwa kama nabii.

Nasema hivyo kwa kuwa mengi ya mambo aliyoyaanzisha kwa ajili ya watu wake maskini, yakiwa na mtazamo wa kustawisha jamii yote bila ubaguzi wa rangi, itikadi, kabila, tabaka, yaliyolenga kuheshimu utu wa watu wote, kuwaona binadamu wote ni sawa na Afrika ni moja, ndiyo anayoyafanya JPM sasa. Y apo mengi, lakini katika mfululizo wa makala haya, nitarejea machache ambayo Mwalimu Nyerere aliyasimamia kama mambo ya msingi ili kuendeleza watu wake maskini na kuwafanya wafaidi matunda ya uhuru waliopigania bila kumwaga damu na kuupata mwaka 1961 na kisha kuungana na Zanzibar mwaka 1964.

Nyerere alitetea maskini, wanyonge, JPM anafanya hivyo moja ya mambo Mwalimu Nyerere aliamini, kuyatenda na kuyasimamia kwa nguvu zote ni kuwasaidia Watanzania maskini na wanyonge wanaoonewa. Katika hili alienda mbali zaidi kuwasaidia hata wa nje wajikomboe dhidi ya ukoloni akiamini Tanzania haiwezi kuwa huru kama Afrika yote haitakuwa huru. Ni katika muktadha huo, tulimwona Nyerere anasaidia nchi za kusini mwa Afrika (SADC) kama Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini, Namibia, Angola kijeshi hadi zinapopata uhuru kamili. Ni yeye pia aliyewasaidia kijeshi Waganda kumtimua nduli Idd Amin alipoivamia Tanzania mwaka 1978.

Kwa kujua umuhimu wa mtu maskini na mnyonge kumiliki ardhi, alitunga sheria inayoifanya ardhi yote ya Tanzania kuwa chini ya R ais na mwananchi kuwa mpangaji ili kila mtu apate. Bila yeye, sehemu kubwa ya ardhi ingekuwa inamilikiwa na matajiri kama ilivyo katika nchi nyingine ikiwamo jirani ya Kenya. Katika nyayo zake, ndimo unapomwona R ais Magufuli akivaa viatu vyake na kutimiza maono hayo na kufanya apendwe kwa kusaidia wanyonge kama alivyodhihirisha Bunda alipomtimua Ofisa Ardhi wa Kanda ya Ziwa kwa kutotekeleza maagizo ya waziri wake kumpa haki bibi kizee aliyeporwa kiwanja.

R ais Magufuli katika maeneo mengi nchini, ameonesha anavyoguswa na kero za maskini, wanyonge na amekuwa akiwaagiza viongozi wanaomsaidia, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, wakurugenzi wa halmashauri za wilaya kila mmoja kusikiliza na kutatua kero za wananchi maskini na wanyonge nchini. Anafanya hivyo akisema hao ndio waliompigia kura na serikali yake imejipambanua kuwatumikia watu hao kwa kupambana na ufisadi, ubadhirifu, wizi, dhuluma, mishahara hewa, ufujaji wa fedha za miradi, rushwa, uvunaji haramu wa rasilimali za nchi na mengine mengi yaliyowanyima haki zao na maendeleo.

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amewasilisha ripoti ...

foto
Mwandishi: Godfrey Lutego

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi