loader
Picha

Waziri: Waliokopa Bodi ya Mikopo wataendelea kukatwa 15%

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema  Serikali haina mpango wa kusitisha makato ya 15% kwenye mishahara ya wanufaika wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu kila mwezi.

Profesa Ndalichako pia amesema, Serikali haijavunja mkataba wowote na wanufaika hao. Ametoa msimamo huo wakati anajibu swali na msingi na swali la nyongeza la Mbunge wa Mbozi, Paschal Haonga.

Katika swali lake la nyongeza, Haonga alitaka kufahamu kama Serikali ina mpango wa kusitisha makato ya mkopo wa asilimia 15 ya mashara ghafi kwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.

Profesa Ndalichako amesema suala la kukata asilimia 15 ya mshahara ghafi kwa wanufaika wa mikopo wa elimu ya juu ni la kisheria na kwamba, Serikali haina mpango wa kusitisha makato hayo.

Kuanzia Januari 2017, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ilianza kukata asilimia 15 ya mshahara ghafi wa mnufaika wa mikopo kutoka kwenye asilimia 8 ya awali baada ya Bunge kupitisha marekebisho ya Sheria ya Bodi ya mikopo mwaka 2016.

Awali HESLB  ilikuwa ikikata asilimia 8 ya mashahara ghafi wa mnufaika kwa kuzingatia tangazo la aliyekuwa Waziri wa Elimu kuanzia mwaka 2011.

Katika swali la msingi, Haonga amesema Bodi ya Mikopo ya Elimu ya imeongeza makato kwa anafufaika wa mikopo kutoka asilimia 8 hadi asilimia 15 bila kuwashirikisha wadau mbalimbali na wanaufaika wa mikopo,

 Je, Serikali haioni kwamba imevunja mkataba kinyume na makubaliano kwa kuwa wakopaji walisaini mkataba wa asilimia 8 na siyo 15?

Haonga pia amesema, ongezeko la makato limewaathiri sana wakopaji na kuwafanya kuwa ombaomba na kuishi maisha magumu sana, je Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kama ni busara kusitisha makato hayo ya asilimia 15 ili kunususru maisha ya watumishi waliokopa.

“Makato ya asilimia 15 kutoka kwenye mshahara ghafi wa munufaika wa mkopo wa elimu ya juu ni ya kisheria yenye lengo la kuhakikisha fedha zinazotolewa a serikali zinarejeshwa kwa wakati ili ziweze kuwasomesha Watanzania wengine wahitaji. Hivyo kwa sasa Serikali haina mpango wa kusitisha makato hayo.” amesema Profesa Ndalichako.

Ametoa mwito kwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu warejeshe kwa wakati mikopo ili watoto wengine wenye uhitaji wakopeshwe.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi