loader
Picha

Wadau kujadili mfuko wa alizeti

Wizara ya Kilimo imesema, Serikali imeandaa mkakati wa kuendeleza zao la alizeti 2016-2020.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Omary Mgumba amesema bungeni kuwa, mkakati huo unalenga kuongeza uzalishaji na tija, kuboresha ubora wa mbegu, kuimarisha tasnia ya alizeti kwa kuboresha utaratibu miongoni mwa wadau, kuchochea ukuaji wa tasnia ya alizeti kwa kuweka sera wezeshi na kuhakikisha kuna masoko ya uhakika kwa mazao ya zao hilo.

Ameyasema hayo wakati anajibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Felister Bura.

Mbunge huyo aliuliza Serikali haioni ni muda mwafaka kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kuanzisha mfuko wa kuendeleza zao la alizeti. Mgumba amesema, bodi hiyo ilianzishwa kufanya biashara na kushirikiana na wadau kuendeleza mazao hivyo haiwezi kuuanzisha mfuko huo bila kushirikiana na wadau wa zao la alizeti.

"Aidha, pale itakapokubalika, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko itakuwa ni mmoja ya wadau muhimu wa kuanzisha mfuko huo" amesema Mgumba.

Amesema, suala la mfuko wa kuendeleza zao la alizeti litajadiliwa kwenye jukwaa la wadau na kama inaonekana ni muda mwafaka wa kuanzisha mfuko huo wadau watakubaliana kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo za uanzishwaji wa mifuko

WANAFUNZI wa kidato cha sita waliopo katika kambi maalum ya ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi