loader
Picha

Wizara- 'Vyuma kukaza' uchumi mzuri

Wizara ya Fedha na Mipango imesema kupatikana kwa fedha kwenye mzunguko si kigezo cha kukua kwa uchumi na kuna madhara makubwa.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Ashatu Kijaji amesema, upatikanaji mkubwa wa fedha kwenye mzunguko ni ishara ya Taifa kushindwa kudhibiti uchumi.

Amempongeza Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BOT) na wataalamu wake kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha hakuna fedha za ziada kwenye uchumi wetu ili tusiingie kwenye matatizo makubwa ya kiuchumi. Dk Kijaji pia amesema bungeni jijini Dodoma kuwa, si kweli kuwa Pato la Taifa limesimama au limeshuka na kwamba, uchumi wa Taifa unakua na watu wa mataifa mengine wanaona.

"Money supply (upatikanaji fedha) kwenye uchumi sio kigezo cha kukua kwa uchumi wa Taifa. Money supply kwenye uchumi inaonyesha kwamba Taifa hilo limeshindwa ku-control (kudhibiti) ukuaji wa uchumi wake. In short run (kwa muda mfupi) unaweza ukajidanganya kwamba ukuaji wa uchumi upo in long run (kwa muda mrefu) matatizo yake na madhara yake ni makubwa sana..."amesema Dk. Kijaji.

Ameyasema hayo wakati anajibu swali la msingi na swali la nyongeza la Mbunge la Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji. Mbunge huyo alitaka kufahamu vigezo sahihi vinavyoanisha ukuaji uchumi wa Tanzania.

Dk. Kijaji amesema kwa mujibu wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa, vigezo sahihi vinavyoainisha kukua kwa uchumi wa nchi yoyote duniani ni ongeeko la Pato la Taifa, ongezeko la pato la wastani la mwananchi kwa mwaka na ongezeko la uuzaji bidhaa na huduma nje ya nchi.

Ametaja vigezo vingine kuwa ni kupungua kwa uagizaji bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi, utulivu wa bei za bidhaa na huduma, utulivu wa viwango vya ubadilishaji fedha za kigeni.

Vigezo vingine ni kuongezeka kwa akiba ya fedha za kigeni na kuongezeka kwa makusanyo ya Serikali kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo na na huduma za jamii.

"Uwekezaji unaofanyika katika nchi ni kigezo kingine cha msingi cha ukuaji wa uchumi kwa kuwa huongeza kasi ya uzalishaji wa bidhaa na huduma, ajira, kipato cha mwananchi mmoja mmoja, pato la Taifa na hatimaye kupunguza umasikini katika jamii" amesema Dk. Kijaji.

WANAFUNZI wa kidato cha sita waliopo katika kambi maalum ya ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi