loader
Picha

CCM yampitisha Kuchauka kugombea ubunge Liwale

Kikao cha Kamati Kuu maalumu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kimempitisha Zuberi Kuchauka kuwa mgombea ubunge wa jimbo la Liwale kwenye uchaguzi mdogo.

Uamuzi huu umewekwa wazi kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole.

Inaelezwa kuwa kamati hiyo ilikaa jijini Dodoma chini ya Rais wa Zanzibar na Makamu wa CCM – Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein.

Kamati hiyo imeagiza Serikali za Tanzania Bara na Zanzibar kuendelea kushughulika na utatuzi wa shida za watu sambaba na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi CCM.

Kikao hicho kimewapongeza wanachama wa CCM na wananchi haswa katika maeneo ya uchaguzi, kwa utulivu, mshikamano na kushiriki katika kutumia haki yao ya kisiasa kuchagua viongozi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na ...

foto
Mwandishi: Na Janeth Mesomapya

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi