loader
Picha

Wastaafu kucheka Ndani ya miezi 6

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Eliud Sanga ameahidi kwamba ndani ya miezi sita, mfuko huo utakuwa umelipa malimbikizo ya madai yote ya wastaafu. Madai hayo ni ya wafanyakazi waliokuwapo kwenye mifuko minne ya PSPF, LAPF, GEPF na PPF ambayo imeunganishwa na kuzaa PSSSF ndani ya kipindi chote cha mchakato wa takribani mwaka mmoja ya kuiunganisha mifuko hiyo.

Sanga alitoa kauli hiyo jijini Dodoma jana wakati wa kuzindua Bodi ya Wakurungezi wa PSSSF, uliofanywa na Waziri wa Nchi, Ofi si ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama. Alisema baada ya kumaliza malimbikizo hayo, mfuko huo utakuwa ukilipa ambapo mdaiwa mafao atakuwa akienda kwenye ofi si za mfuko huo na kunywa chai wakati akisubiri mafao yake badala ya kusubiri kesho.

Sanga alisema tayari mfuko huo, umeshaapisha watendaji wa ofi si za mikoa 26 Tanzania Bara na mmoja wa Visiwani. Alisema wiki ijayo wanaanza kazi ya mfuko huo, ikiwa ni pamoja na kuhakiki wanachama waliopo katika mikoa yao. Wastaafu sasa kucheka ndani ya miezi 6 INATOKA UK.1 Wanatakiwa kufahamu wastaafu wote tangu mwezi Julai mwaka huu na kuwaandalia mafunzo ya kustaafu kabla hawajastaafu ili kuhakikisha hawafi mapema au hawafi kabisa.

Akizindua Bodi hiyo, Jenista aliwataka watendaji wa mfuko huo, kutofumbia macho mfanyakazi yoyote atakayeshindwa kutimiza wajibu wake wa kutoa huduma nzuri kwa wadai wa mafao hayo mahali popote. Aliwataka watendaji hao waangalie miradi zaidi ya 16, iliyokuwa ikitekelezwa na mifuko minne iliyounganishwa na kuhakikisha kama inafaa na kama ina manufaa kwa taifa, basi waiendeleze au kuifufua. Pia aliwataka wafanye kazi kuongeza wanachama, kwani mifuko hiyo kwa umoja ilikuwa na wanachama asilimia 11 ya wafanyakazi wote, hivyo lazima wafi kie malengo ya kuwa na wanachama asilimia 40 ifi kapo 2025.

Alimtaka Mkurugenzi Mkuu kuhakikisha anatekeleza ahadi yake ya kwamba ifi kapo F ebruari mwakani, wafanyakazi wastaafu watakuwa wanafi ka ofi si za mfuko na kupewa chai wanywe wakati wanasubiri mafao yao badala ya njoo kesho njoo kesho. Akizungumza Mwenyekiti wa Bodi, Mussa Iyombe alisema bodi ni nzuri na wamejipanga kuhakikisha kero zilizokuwa zikiwakumba wastaafu, zimalizika ndani ya kipindi cha miezi sita, kama Mkurugenzi Mkuu, Sanga alivyoahidi.

Iyombe ambaye ni Katibu Mkuu Tamisemi, alisema wanataka kuondoa kero ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikililalamikiwa na wastaafu, ambao wamekuwa wakifuata mafao yao. Alisisitiza kwamba ndani ya kipindi kifupi, kero hizo zitakuwa historia. Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), Tumaini Nyamhokya alisema wao ndio walikuwa wapiganiaji wa mifuko hiyo kuunganishwa. Lakini, alisema halikuwa jambo rahisi kuunganisha mifuko na hatimaye jana kuzinduliwa bodi hiyo.

Nyamhokya aliwataka watendaji wa mfuko huo, kuweka kipaumbele kwa wanaostaafu kulipwa mafao yao kwa lengo la kuanzisha shughuli mbalimbali katika maisha yao. Akitoa neno la shukrani, Rais wa Chama Cha Walimu (CWT), Leah Ulaya alisema wapo tayari kufanya kazi kwa weledi. Aliahidi kuwa hawatamuangusha waziri, wizara na wanachama wa mfuko huo. Leah ambaye ni mjumbe wa bodi hiyo, alisema wamejipanga kumshauri waziri na watahakikisha wanamshauri vizuri. Kwa sasa kutakuwa na mifuko minne, ukiwemo Mfuko wa NSSF kwa ajili ya sekta binafsi, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mfuko wa F idia Kwa Wafanyakazi (WCF) na PSSSF.

TIMU ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, imerejea katika fainali ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi