loader
Picha

Watu 35 kortini kwa ushoga, ukahaba

JUMLA ya watu 35 wamefi kishwa mahakamani wakituhumiwa kujishughulisha na vitendo vya ukahaba pamoja na mapenzi ya jinsia moja ambavyo ni kinyume cha utamaduni wa watu wa Zanzibar.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Shamata Shaame wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kufahamu operesheni ya kuwatafuta watu wanaofanya biashara ya ukahaba zimefikia wapi.

Akifafanua zaidi, Shaame alisema operesheni ya kusaka watu wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili yao ni kinyume cha mila na utamaduni ambayo katika awamu ya kwanza imepata mafanikio makubwa.

Alikiri kuwepo kwa kasi ya matukio ya vitendo vya ukahaba ambavyo kwa kiasi kikubwa vimechangiwa na kuwepo kwa nyumba za starehe na vilabu vinavyofanya biashara ya pombe.

“Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa inaendelea kusaka watu wanaokiuka mila na utamaduni na kujishughulisha na vitendo vya ukahaba katika mikoa yote nchini ambapo katika hatua za awali limepata mafanikio makubwa,” alisema.

Hata hivyo, Shamata alikiri ugumu wa utekelezaji wake ambapo hufanyika kwa usiri na unyeti mkubwa. Alisema kusaka watu wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili ni endelevu kwa ajili ya kulinda mila na utamaduni pamoja na silka ya wananchi wa Zanzibar

HALI ni tata katika mji wa Namanga mpakani mwa Tanzania ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi