loader
Picha

Mnada wa kahawa kufanyika Bukoba

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewatangazia wakulima wa kahawa Kagera mnada wa kahawa utafanyika mkoani humo kupunguza gharama kwenda Moshi, Kilimanjaro.

Akizungumza na wadau wa kahawa, wakulima, wanunuzi wa kahawa, wamiliki wa viwanda vya kahawa jana alisema mara nyingi vyama vya msingi vimekuwa vikijiwekea tozo mbalimbali ikiwemo kusafirisha kahawa kwenda Moshi.

Alisema mkakati wa serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata stahiki yao ya mazao wanayoyauza huku akisema serikali iko tayari kubadili mfumo wakulima waweze kunufaika. Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa kwa sasa vyama vya ushirika ndivyo vinavyoongoza kuwaibia wakulima.

Alisema licha ya serikali kufuta tozo nyingi, bado vyama vya msingi vinajiongezea tozo ili kuwaibia tena wakulima.

“Kagera tunavyama viwili vya ushirikika KCU na KDCU lakini vyama hivi vimejiongezea tozo vyenyewe ili kuwaibia wakulima mpaka sasa KCU ina tozo 20 na KDCU ina tozo 18 je, hizi tozo zinatoka wapi wakati zilishafutwa nawahakikishia nyote mtaishia jela,” alisema.

Alisema mkutano wake ni wa kuimarisha zao la kahawa na akawataka wafanyabiashara kununua kahawa yote iliyobaki ili kuwapatia fedha zao akikemea vyama vya msingi kukaa na kahawa za wakulima miezi mitatu bila kulipa fedha zao.

Amesema sasa taifa linaelekea uchumi wa kati hivyo viwanda ambavyo vinaongeza thamani ya mazao vitapewa kipaumbele kwani mara nyingi mazao yasiyoongezewa thamani hushusha bei.

Alisema kutokana na vyama vya msingi kukopa fedha kwa jina la wakulima na kuilimbikizia serikali madeni kwa kukopa mikopo benki, serikali ya awamu ya tano haitarithi madeni ya vyama vya msingi hivyo atakayekopa atalipa.

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Charles Tizeba alisema Kagera ilipaswa kukusanya kahawa tani 81,000 ya kahawa safi, lakini mpaka sasa tani 50,000 zimekusanywa na wakulima wameficha kahawa zao kutokana na kutolipwa fedha zao kama malipo ya awali.

Rais John Magufuli amewakaribisha wananchi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya ...

foto
Mwandishi: Diana Deus, Bukoba

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi