loader
Picha

Shime- Kazimoto bado yupo sana

WAKATI mashabiki wengi wakimpigia hesabu kiungo wa JKT Tanzania Mwinyi Kazimoto kama siyo mwisho wa msimu huu basi msimu ujao anatundika daluga, suala hilo limepingwa vikali na kocha wake, Bakari Shime akieleza kiungo huyo bado ‘mbichi’ kabisa kutokana na shughuli anayoifanya.

Shime amefunguka kuwa moja ya wachezaji wenye msaada mkubwa kwa sasa katika timu yake ya JKT ni Kazimoto ambaye ametumika katika michezo yote saba iliyocheza timu hiyo bila kufungwa mpaka sasa.

Alieleza zaidi, kutokana na nguvu, uwezo na aina ya uchezaji wake anaamini kiungo huyo bado ana nafasi ya kucheza zaidi ya miaka mitano na akawazidi wengi wanaochipukia kwa kuwa anamfahamu vizuri mchezaji huyo hivyo hadhani kama anaweza akuondoka kwenye uso wa soka kwa sasa.

“Mwinyi anafanya mambo mengi ndani ya timu kama vile chipukizi, anapambana na ana mchango mkubwa kwa timu katika mechi zote hizi. Sidhani kabisa kama ataondoka kwa sasa kwenye soka, mimi ndiyo namuona kila wakati hivyo nafahamu juu ya uwezo wake...

“Anaweza kucheza soka zaidi ya miaka mitano mbele, na kutokana na uwezo wake bado ana nafasi kubwa ya kurejea tena katika kikosi cha timu ya taifa, kikubwa ni nafasi tu lakini Mwinyi bado kabisa,” amesema Shime ambaye leo ataiongoza JKT dhidi ya Alliance.

Kazimoto ni moja ya viungo wakongwe nchini waliong’ara kwa takriban miaka 10 iliyopita, akianza kuonekana kupitia JKT kabla ya kujiunga na Simba na baadaye kutimkia Al-Markhiya ya Qatar. Msimu wa mwaka 2015-16 alirejea tena Simba kabla ya mwanzoni mwa msimu huu kujiunga tena na JKT.

KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mnigeria ...

foto
Mwandishi: Hans Mloli

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi