loader
Picha

Rwanda kuandaa mkutano Madola

SHIRIKISH O la Michezo ya Jumuiya ya Madola (CG F) limeitangaza Rwanda kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa C G F utakaofanyika mwakani.

Mkutano huo utafanyika mjini hapa Septemba 4 hadi 8, 2019. Pia watakuwa wakikumbuka miaka 10 tangu Rwanda ilipojiunga na Jumuiya ya Madola mwaka 2009, na mwaka mmoja baadae, Rwanda wataandaa Mkutano wa Kiserikali (C H O G M) mwaka 2020.

Rais wa C G F, Louise Martin alisema: “Uanachama wa Rwanda katika Jumuiya ya Madola ni wa aina yake na tunakaribisha nafasi hii kusherehekea pamoja na wanachama chipukizi katika familia yetu ya michezo.

Rwanda ni nchi ya kuvutia, na yenye uongozi mzuri wa michezo na wanaangalia mbele na kitendo cha kuandaa mkutano wa C G A bila shaka kutaiongeza hamasa ya kuendelea kufanya vizuri katika michezo.” Mbali na hayo, Rais wa C hama cha Michezo ya Jumuiya ya Madola cha Rwanda, alisema: “Tuna heshima kubwa kuchaguliwa kuwa wenyeji wa mkutano mkuu wa C G F 2019.

Tunataka kutumia nafasi hii muhimu kujenga jina la Rwanda, na zaidi Jumuiya ya Madola. Rwanda imekuwa kituo cha kufanyikia mikutano ya kimataifa, na wajumbe watakaoshiriki mkutano huo watashuhudia jinsi jiji la Kigali lilivyo, na kuwa kitovu kikubwa cha uchumi wa Rwanda, ambao ni fahari kwa kila Mnyarwanda.”

Mkutano huo mkuu utafanyika katika ukumbi wa Kigali C onvention C entre, ambapo ajenda kubwa itakuwa Uchaguzi Mkuu wa C G F, kupitia sheria zinazoongoza C G F na kanuni zake.

Rwanda ilianza kushiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola katika michezo ya 2010 iliyofanyika Delhi, India na kupeleka timu za riadha, ngumi, baiskeli na kuogelea, ambapo walishinda medali yao ya kwanza katika Michezo ya Jumuiya ya Madola ya vijana iliyofanyika Bahamas 2017 wakati walipotwaa medali ya shaba katika mchezo wa wavu wa ufukweni kwa wanawake.

Wakati wa Michezo ya Jumuiya ya Madola iliyofanyika G old C oast, Australia 2018, nchi zote zilizoshiriki zilisimama kimya kwa dakika moja ili kutoa heshima kwa zaidi ya watu milioni 1 waliopoteza maisha katika mauaji ya kimbari 1994 dhidi ya Watutsi. Utakuwa Mkutano Mkuu wa pili kufanyika barani Afrika katika kipindi cha miaka saba, ambapo Kampala, Uganda ndio iliandaa mkutano wa mwaka 2012.

KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mnigeria ...

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi