loader
Picha

Klabu England zapigana kumbo kwa Samatta

HABARI Njema kwa mshambuliaji wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars Mbwana Samatta anayechezea katika Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, ni kutakiwa na klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England ikiwemo Everton.

Mbali na Everton, klabu nyingine zinazowania saini ya nyota huyo ni Burnely,Westham na Brighton. Samatta ambaye ni mchezaji bora barani Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani mwaka 2016, amekuwa akionesha kiwango kizuri toka msimu huu uanze ambapo mpaka sasa amefunga mabao 14 katika mechi 16 alizocheza kwenye michuano yote.

Na katika mechi hizo Samatta amefunga ‘hat trick’ mbili, moja akifunga katika Ligi ya Ubelgiji na nyingine akifunga katika michuano ya ligi ya Europa. Akizungumza na gazeti hili jana, wakala wa mchezaji huyo Jamal Kisongo alisema kuwa kwa sasa hizo ni tetesi na kwamba mambo yatajulikana baada ya dirisha la usajili kufunguliwa.

“Saahizi mawakala wanafanya kazi ya kuangalia wachezaji tofauti kwa mahitaji ya klabu zao hivyo kupata uhakika kama mchezaji anawaniwa na klabu fulani tusubiri hadi muda wa dirisha la usajili ukifika,”alisema Kisongo.

KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mnigeria ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi