loader
Picha

Wizara zaungana kukabili ukatili, ndoa kwa watoto

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais- TAMISEMI zimedhamiria kuimarisha na kuyaongezea nguvu madawati ya malezi shuleni ili kuweza kuwaweka wanafunzi huru zaidi kutoa tarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk. John Jingu aliyasema hayo jijini Dar es Salaam leo Alhamisi katika mdahalo wa kitaifa kuhusu ndoa za utotoni na ukeketaji ulioandaliwa na wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), pamoja na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania(TAMWA).

“Tayari walimu wa malezi wapo katika shule zote, lakini tutakachofanya ni kuyaimarisha madawati hayo ili yaweze kusimamia na kushughulikia masuala haya ya ukatili wa kijinsia, tunaamini wanafunzi wakipewa elimu ya kutosha wanaweza kutoa taarifa za kina endapo watafanyiwa au watashuhudia vitendo vya ukatili” alisema.

Alisema, serikali inafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha wanabadilisha fikra hasi ili kuhakikisha mtoto analindwa na katika kukabiliana na ukatili sambamba na kupambana na ndoa na mimba za utotoni zipo sheria mbalimbali zimewekwa ili kuhakikisha wanamlinda mtoto kwa vitendo.

Alisema chanzo cha ukatili kwa watoto ni pamoja na mila potofu, fikra na imani za watu, umaskini na tamaa ya mali na kwamba serikali imejiwekea mikakati mbalimbali ua kukabiliana na jambo hilo.

“Tunachopaswa kujiuliza ni kwanini tunafanya vitendo hivi? Tunathamini utamaduni wetu ila kuna tamaduni nyingine zinaleta maumivu na ni ukatili kwa jamii zetu na hivyo kuathiri mambo mengi ikiwemo mfumo wa elimu na kuendeleza umaskini” alisema.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dodoma, Fatma Toufiq alisema mkoa wao ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa ndoa za utotoni lakini wameanzisha kauli mbiu ya 'magauni manne kwa mtoto wa kike', ikiwemo sare ya shule, joho la kumaliza shule, gauni la harusi na gauni analovaa mjamzito.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima alisema ukatili wa wanawake na watoto umejificha chini ya mila, desturi na tamaduni na kusema kwamba ushirikiano unahitajika kumaliza tatizo hilo kwa kuwa hakuna mwanamke anayependa kupigwa wala mtoto anayependa kuolewa bila kusoma.

Naye Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Kivulini, Yassin Ally aliwataka wazazi na walezi kutoa mahitaji kwa watoto wao ili wasishawishike kwa kuwa wamebaini kwamba wengi wanaojiingiza kwenye mapenzi katika umri mdogo wengine wanashawishiwa na fedha kulingana na mahitaji yao.

TIMU ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, imerejea katika fainali ...

foto
Mwandishi: Hellen Mlacky

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi