loader
Picha

Mafunzo kutoka Veta kuchagiza uchumi-Ole Nasha

VIJANA wanaopitia elimu ya mafunzo ya ufundi stadi (VETA) wanamchango mkubwa katika uanzishaji wa sera ya viwanda nchini kupitia mafunzo yanayofundishwa ya nadharia na vitendo.

Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia, William Ole Nasha aliyasema hayo wilayani Babati wakati akitembelea chuo cha VETA mkoani Manyara kujionea shughuli zinazofanywa katika chuo hicho.

Alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kila mkoa unakuwa na chuo cha VETA na pia kwa kila Wilaya na kwa mikoa ambayo bado haina vyuo hivyo itawalazimu kujenga mikoa kama Rukwa, Geita na Njombe.

Kupitia azma hiyo ya serikali itasaidia kupata nguvu kazi katika uchumi wa viwanda pia ni fursa ya kuwajengea vijana wengi ambao hawakuweza kupokelewa kwenye mfumo wa elimu ya juu kutokana na ongezeko kubwa la vijana wanaomaliza masomo.

TIMU ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, imerejea katika fainali ...

foto
Mwandishi: Theddy Challe, Babati

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi