loader
Picha

Stars itashinda -Mwakyembe

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema ana hakika timu hiyo itarejea na ushindi kutoka Cape Verde.

Stars ilisafiri alfajiri ya jana kwenda Praia kucheza na wenyeji wao Cape Verde kesho mechi ya kuwania kufuzu fainali za michuano ya Kombe la Mataifa Afrika iliyopangwa kufanyika Cameroon mwakani.

Stars na Cape Verde zipo kundi moja na Uganda na Lesotho na tayari kila timu imecheza mechi mbili huku Uganda ikiongoza msimamo wa kuwa na pointi nne, ikifuatiwa na Tanzania yenye pointi mbili.

Akizungumza kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam saa chache kabla timu hiyo haijaondoka, Mwakyembe alisema ameamua kuacha usingizi wake na kwenda kuwasindikiza kutokana na kuwa ana uhakika wa asilimia zote kuwa watarudi na ushindi hivyo wasimuangushe.

Kwa upande wa serikali, kiongozi aliyeambatana na Stars ni Mkurugenzi wa Michezo, Yusuf Singo. Mwakyembe aliwataka wachezaji hao kutambua kuwa serikali pamoja na watanzania kwa ujumla wapo nyuma yao hivyo wasiwaangushe na pia kama alivyofanya kuwasindikiza hivyohivyo anatarajia kufanya pia wakati watakaporudi hivyo wanapaswa kuhakikisha wanapata ushindi ili awapokee kwa furaha.

Aliwasisitiza kuhakikisha wanakabiliana na wapinzani wao kwa kujiamini na kujituma licha ya kuwa ugenini wakijua fika kuwa wanapigania taifa lao ambalo limepoteza heshima kwenye michuano hiyo kwa miaka 38 sasa tangu kushiriki fainali ikiwa ni mara ya kwanza na mwisho.

“Nyie ndio tumaini la Tanzania kuturejeshea heshima iliyopotea kwa zaidi ya miaka 38 haijapata kutokea ni muda mrefu mno, sasa tumechoka, nina uhakika tuna kikosi kizuri sana, benchi la ufundi zuri sana lenye weledi wa kila aina…

“Sisi kazi yetu kubwa kuwatia moyo na kuwaombea kwa Mungu mfike salama na vilevile tarehe 12 muoneshe mchezo wa kujiamini, kujituma kupigania taifa lenu mimi nina uhakika moyo wangu hauna dukuduku kabisa najiandaa kuwapokea mkirudi,” alisema Mwakyembe.

KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mnigeria ...

foto
Mwandishi: Mohammed Mdose

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi