loader
Picha

TaSUba yatamba kufanikiwa

TAASISI ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imesema lengo la kuanzishwa kwake mwaka 1981 limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mtendaji Mkuu wa Tasuba, Dk Herbert Makoye amesema jana Jijini Dar es Salaam kuwa TaSUBa tangu ianzishwe imepata mafanikio mengi ikiwemo kutoa wataalamu mbalimbali.

Alisema hayo katika mahojiano na kipindi cha 360 kinachorushwa Kituo cha Luninga Clouds. Alisema Tasuba imetoa maofisa utamaduni na sanaa wanaofanya kazi halmashauri za wilaya, manispaa, majiji na sekretarieti za mikoa.

Aidha alisema Tasuba imetoa watendaji wakuu wa taasisi za serikali kama Bodi ya Filamu na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na maprofesa wanaofundisha vyuo vikuu ndani na nje na wasanii wa muziki na fani nyingine za sanaa.

“Nasema hayo kufafanua ‘clip’ inayozunguka ambayo hata mimi nimeiona inayotokana na shughuli iliyofanyika Tandale ikidai TaSUBa wanalipwa mshahara wa bure,” alisema.

“Jambo hilo ni la hatari ndio maana nimechelea kukutajia majina. Hiki chuo kilianzishwa mwaka 1981 kikiwa na malengo yake na sidhani kama kuna chuo kinaanzishwa kwa lengo la kutengeneza celebrities (wasanii nyota).

Kwa kufanya hivyo basi tungekuwa tunachukua wanafunzi wawili tu. TaSUBa inatoa nafasi kwa vijana wote kujifunza sanaa na wanapofika kila mtu anachagua anachokitaka wengine kuwa waandishi wa filamu au waimbaji, ’’alisema.

Akielezea historia ya chuo, Dk Makoye alisema ilianza mwaka 1962 baada ya uhuru ambapo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alianzisha Wizara ya Utamaduni lengo likiwa ni kulinda utamaduni wa Mtanzania ambao ulikuwa umeharibiwa kipindi cha ukoloni.

KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mnigeria ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Bagamoyo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi