loader
Picha

Mabadiliko tabianchi tishio Zanzibar

JUMLA ya maeneo 150 yameathirika na mabadiliko ya tabianchi Unguja na Pemba, huku baadhi ya wananchi wakisitisha shughuli za kilimo.

Ofisa wa Idara ya Mazingira Mwalimu Khamis Mwalimu amesema visiwa vya Unguja na Pemba vipo katika tishio la mabadiliko ya tabianchi kutokana na kasi ya maji ya bahari kuvamia maeneo ya makazi katika maeneo ya fukwe.

Amesema baadhi ya wananchi wamevihama visiwa vidogo vilivyopo Pemba ikiwemo Kisiwa Panza na Mtambwe Mkuu kutokana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ya maji ya bahari kuvamia maeneo ya makazi.

“Visiwa vya Zanzibar vinakabiliwa na athari ya mabadiliko ya tabia ya nchi kutokana na kasi ya maji ya bahari kuvamia maeneo ya makaazi ambapo chanzo kikubwa ni uharibifu wa mazingira,” amesema.

Akiendelea kuzungumzia athari za mabadiliko ya tabia nchi, alisema hivi sasa baadhi ya wananchi wamekuwa wakichota mchanga wa pwani kwa ajili ya matumizi ya ujenzi wa nyumba.

Alisema kwa mujibu wa sheria za mazingira ni marufuku kwa wananchi kuchota mchanga wa kwa matumizi ya kazi za ujenzi ikiwemo kupiga matofali.

''Lipo tangazo linalopiga marufuku wananchi kuchota mchanga katika maeneo ya fukwe kwa kazi za ujenzi au kupiga matofali,''amesema.

Alifahamisha kwamba baadhi ya maeneo yaliyoathirika na athari za mazingira yamesababishwa na wananchi kuchota mchanga wa pwani na hivyo kuruhusu maji ya baharini kuingia katika maeneo ya makaazi.

Mkurugenzi wa Kamisheni ya Mazingira Zanzibar Sheha Mjaja amesema, Serikali imeanza kuhamasisha vikundi vya mazingira kuotesha miti aina ya mikoko kwa wingi kwa ajili ya kuhifadhi athari za kimazingira.

Zaidi ya miti ya mikoko 26,000 imeoteshwa katika eneo la msitu wa hifadhi ya Jozani Unguja ikiwa ni sehemu za juhudi za kupambana na athari za kimazingira na kuzuia kasi ya maji ya chumvi kuingia katika maeneo ya makaazi ya wananchi.

''Njia pekee ya kukabiliana na athari za mazingira ni kuotesha kwa wingi miti aina ya Mikoko ambayo moja ya sifa yake kubwa kuzuwia kasi ya maji ya chumvi ili yasilete madhara''amesema.

TIMU ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, imerejea katika fainali ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi