loader
Picha

Wanafunzi walazimisha kuolewa

SERIKALI imetakiwa kuwachukulia hatua wasichana wanaokatisha masomo ili waolewe, hali itakayosaidia kupunguza tatizo la mimba na ndoa za utotoni katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Chilonwa wameyasema hayo wakati wakipewa elimu juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia, mimba na ndoa za utotoni ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi unaohusiana na kutokomeza ukatili wa kijinsia, mimba na ndoa za utotoni unaotekelezwa na Shirika la Woman Wake Up ( WOWAP) kwa ufadhili wa The Foundation for Civil Society.

Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule hiyo, Lameck Mwinjari alitaka kuchukuliwa kwa hatua kwa wasichana wanaoolewa chini ya miaka 18.

"Msichana chini ya miaka 18 anaporidhia kuolewa anachukuliwa hatua gani, maana kuna wengine wanaacha shule au kupata mimba wakiwa shuleni ili waolewe,"amesema.

Akijibu hoja hiyo, Muelimisha Rika kutoka Kijiji Cha Mahama, Stella Madelemu amesema kama mtoto anang'ang'ania ndoa katika umri mdogo, mzazi ana haki ya kumshitaki.

“Mzazi anaweza kumshtaki mtoto wake ili aachane na dhamira yake ya kuolewa katika umri mdogo,"amesema.

Amesema ndoa za utotoni ni pale mtoto anapoolewa akiwa na umri chini ya miaka 18 na ndoa hizo zina madhara hasa pale binti anapobeba mimba.

Mwanafunzi mwingine, Benjamin Yoram alisema baadhi ya wazazi wamakuwa wakiwaoza watoto wao wenye umri mdogo kwa sababu ya kupata mahari.

"Ni zipi njia sahihi za mtoto anazotakiwa kufuata kama analazimisha kuolewa na msaada gani atapata ili aondokane na janga hilo?'' alihoji mwanafunzi huyo.

Akijibu hoja huyo, muelimisha rika Christopher Malogo alisema mtoto anaweza kuongea na wazazi.

"Ukiona mzazi hakuelewi waelimisha rika wapo nenda kawaone ili watoe ushauri katika familia ile,"amesema.

Mratibu wa mradi huo, Nasra Suleiman kutoka WOWAP alisema wamekuwa wakitekekeza mradi huo na watoto wa kike wamekuwa wahanga wa mimba na ndoa za utotoni.

"Mtoto wa kiume ana nafasi kubwa ya kumlinda mtoto wa kike kwa sababu mimba nyingine zinatokana na watoto wa kiume walio shuleni,"alisema.

Amesema wataendelea kutoa elimu katika suala la kujitambua ili kutokomeza mimba za utotoni.

Amesema elimu inatolewa katika maeneo mbalimbali ni vyema kama wanafunzi wakazingatia masomo na kuacha kujiingiza kwenye ngono wakiwa katika umri mdogo mdogo waweze kufikia malengo yao.

TIMU ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, imerejea katika fainali ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Chamwino

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi